Wednesday, 10 August 2011

Ziara ya Parapanda Swedeni


 Mgunga Discussion with Zodi ,the costume designer on her designs
 Eva (Antigone) in rehearsal
 The  Production Directors
 Mgunga Presenting Parapanda actors to the swedish counterpart actors
 The  Production Directors Mgunga mwa Mnyenyelwa of  Parapanda Theatre and  Ronny Hallgren 



 The Gothernburg City Theatre  building
        Wasanii 7 na Mwongozaji mmoja wa kundi la sanaa za maonyesho la Parapanda wako nchini Sweden kwa ziara ya maonyesho  ya Utambaji wa mashairi na uandaaji wa  tamthiliya ya ANTIGONE. Tamthiliya hii imeandikwa miaka 42 kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita. Mwandishi  wake ni  Yule msanii mwandishi nguli wa kigiriki wa tamthiliya za jukwaani aliyejulikana kwa jina la  Sophocles.

Tamthiliya hii  imetafsiriwa katika lugha  zote kuu za dunia  kasoro Kiswahili na kwa mara ya kwanza itachezwa kwa Kiswahili na Kiswidi.

Maandalizi na maonyesho ya tanthiliya hii yanafanywa na taasisi mbili za sanaa za maonyesho: Parapanda Theatre Lab Trust na Gothernburg City Theatre ya Swideni .kuanzia  tarehe 2/8/2011 mpaka 14/12/2011. Maandalizi na maonyesho yanafanyika Swideni  na Tanzania.

Majina ya wasanii na Waongozaji











Wasanii wa Parapanda
Wasanii wa Gothernburg Theatre

Jane Mwatonoka
Nina Zanjani

Frank Samatwa
Johan Karlberg

Daud Joseph
Fredrik Evers

Shabo Makota
 Anna Bjelkerud

Amani Lukuli


Habiba Nguogani


Eva Nyambe





Waongozaji
 Tamthliiya hii  inaongozwa(directed)  na  Mtaalamu na muongozaji maarufu wa tamthilya za jukwaani Mgunga mwa Mnyenyelwa wa Parapanda Theatre na   bwana Ronny Hallgren mwongozaji mashuhuri wa tamthliya  nchini Swedeni. Bwana  Ronny pia ni  Mkurugenzi wa jumba la maonyesho la sanaa  la jiji la Gothernburg.
Kuhusu Mahusiano
 Ushirikiano huu ulianza miaka  takribani 10 iliyopita ikiwa ni matokeo ya mradi wa PACSEA ( Performing Arts Coorperation Between Sweden and East Africa) ambao ulikuwa ni ushirikiano baina ya Uswidi na nchi za  Masharik mwa afrika; Kenya,Tanzania,Uganda na Ethiopia .( Mradi  huu  uliokuwa unaratibiwa na taasisi ya sanaa kusini mwa afrika –EATI kwa ufadhili mkubwa na SIDA, ulifikia kikomo mwaka 2009.

Wakati wa mradi huu vikundi na taasisi za sanaa za maonyesho kutoka nchi za mashariki mwa Afrika  ziliweka urafiki na wasanii wa vikundi na taasisi za Uswidi. Katika Mahusiano hayo vikundi vilitembeleana,vikafanya warsha na kushiriki katika  matamasha ya Uswidi na Tanzania.
 Ni wakati huu ndipo taasisi ya sanaa ya Prapanda Theatre Lab Trust ilipopata rafiki kutoka Uswidi ambayo ni taasisi ya kuandaa na kuonyesha tamthiliya ya serikali ya jiji la Gothernburg kwa jina la Gothernburg City Theatre.

Parapanda & Gothernburg City Theatre.
Chimbuko la mahusiano ya taasisi hizi mbili  ni Tamasha la  Sanaa la EATI lilifanyika  Mombasa Kenya. Mkurugenzi wa GCT mr Ronnie Heglen alifika kutoka Swideni na kushuhudia onyesho la “Kalunde” ambalo lilikuwa ni mchanganyiko wa utambaji wa hadithi, muziki na ushairi. Uongozi wa kutoka Jumba la sanaa la Gothernburg  ulikaa kikao na uongozi wa Parapanda  chini ya bwana Mgunga  Mwa Mnyenyelwa  kuhusu nia ya kuanzisha ushirikiano wa kisanii.

Ushirikiano huu uliwasilishwa rasmi katika vikao vya PACSEA na EATI  na kukubaliwa.
Hatua ya awali katika ushirikiano huo ika ni  kuwa  na warsha ya kutambuana na kubadilishana mawazo . Warsha hii ilifanyika  mwaka 2005 katika ofisi za Parapanda. Wasanii sita kutoka GCT walikutana na wasanii nane wa Parapanda  kwa muda wa wiki moja. Ni katika warsha hii ambapo  wasanii wa Parapanda walionyesha  hazina waliyonayo katika sanaa.Warsha kama hiyo ikafanyika mwaka 2008 nchini Uswidi. Halikadhalika huko wasanii wa Parapanda walijifunza mbinu na aina ya sanaa inayofanywa na GCT.

Wasanii wa Parapanda  walishiriki katika matamasha ya Utambaji hadithi na ushairi  nchini Swideni mara mbili; 2005 na 2007.Baada ya kufahamiana vizur,i  Uamuzi wa kuandaa onyesho la pamoja ulifanyika. Mapendekezo   yalitolewa na GCT kwamba  tamthiliya ya Antigone  ndiyo ingefaa kuandaliwa. Sababu kubwa ilikuwa; ni tamthiliya kongwe inayoheshimika duniani na pili ni tamthiliya  inayoeleza masuala kadhaa  ambayo yanaakisi maisha ya leo ya sehemu nyingi duniani ikiwemo Tanzania. Suala kubwa ni Harakati za Mwanamke kupambana na mifumo gandamizi, wajibu wa raia, migogoro ya kitabaka na kiutamadini na  nafasi ya vijana katika jamii inajitokeza.
    
  Uamuzi  wa kuandaa tamthiliya hii ulikubaliwa na Parapanda na kuanza kuandaa ratiba ya utekelezaji . Kwa mujibu wa mradi huu, wasanii saba wa Parapanda  na wanne wa GCT watachukua husika. Kutakuwa na waongozaji wawili, Mgunga Mwa Mnyenyelwa (Parapanda) na Ronnie Hegllen (GCT). Onyesho litatumia  sehemu kubwa ya mbinu za uwasiishaji za Parapanda husussani katika muziki,ngoma na ushairi.

Ratiba ya maandalizi na maonyesho












Tarehe
 Tanzania
Juni 31
 Kuondoka kwenda Swideni  kuandaa onyesho
Agosti 28
 Kurudi Tanzania na kuendelea na maandalizi
 Sept 21
 Ufunguzi wa onyesho Tanzania
Sept 22- 25
  Maonyesho Tanzania. Waterfront, Kituo cha Utamaduni cha Urusi – 22/9   wazi, 23/9 wanafunzi

-          tamasha la sanaa Bagamoyo: 25/9
 Sept 29
 Kwenda  Swideni
Oktoba  8
 Kufungua maonyesho Swideni
Desemba  14
 Kumaliza maonyesho   Swideni
Desemba 16
 Wasanii kurudi nyumbani.
                        Jumla ya maonyesho swideni 28
   2.   Kushiriki Tamasha la Utamaduni  Jiji la Gothernburg
  Wakati wa ziara hiyo Parapanda mealikwa kufanya maonyesho ya  muziki na utambaji wa mashairi  na ngoma katika tamasha la Utamaduni la watu wa Gothernburg wiki ijayo tarehe 19/8/2011 usiku katika uwanja maarufu wa maonyesho ya nje wa  Gothernburg City . Makundi mbalimbali zaidi ya ishiriki kutoka ndani na nje ya Swideni yantarajiwa kushiriki. Wasanii wa Parapanda wapo katika mazoezi makali ya kushiriki tamasha hilo sambamba na  maandalizi ya tamthliya ya Antigoni

 Mgunga Mwa Mnyenyelwa
 Mwongozaji &Mkuu wa msafara.

No comments:

Post a Comment