Monday, 2 August 2010

matokeo kura za maoni CCM hadi sasa

Miongoni mwa wanasiasa mahiri na wakongwe walioangushwa ni Mbunge wa Mtera, John Malecela, ambaye ameliongoza jimbo hilo kwa miaka zaidi ya 25, ambapo amekwaa kisiki kutoka kwa Katibu wa UVCCM wilaya ya Tarime, Livingstone Lusinde.

Mzee Malecela alipata kura 3,326 katika kata 13 kati ya 19 wakati mpinzani wake Lusinde amepata kura 3,375.

Hata hivyo, Lusinde alifika katika ofisi za katibu huyo na kudai amekamilisha matokeo ya kata zote na ameshinda kwa kupata kura 5,810 wakati Malecela ana kura 5,379 .

Barongo alisema katika jimbo la Mpwapwa, mbunge wa zamani George Lubeleje alipata kura 4,830 huku mpinzani wake Gregory Teu akipata kura 7,777.

Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, aliibuka kidedea katika kata 13 kati 16 baada ya kupata kura 8,824 huku mpinzani wake Aggrey Galawika akiwa na kura 2,537.

Kwa upande wa jimbo la Chilonwa, Ezekiah Chibulunje alipata kura 5,269 katika kata nane kati ya kata 13 wakati mpinzani Mwaka Joel akipata kura 3,848.

Kondoa Kaskazini Zabein Mhita aliibuka mshindi katika kata 15 kati ya kata 28 kwa kupata kura 6,211 huku mpinzani wake Mohamed Moni akiwa na kura 2,116.

Kondoa Kusini Juma Nkamia alipata kura 4,249 katika kata 11 kati ya 20 wakati mkongwe Pascal Degera akipata kura 632.

Jimboni Bahi, Dinald Majitii aliongoza kwa kupata kura 2,627 katika kata 15 kati ya 24 huku mgombea mwenzake Omar Badwel akipata kura 2,268.

Kwa upande wa jimbo la Kongwa, Job Ndugai ameibuka kidedea baada ya kupata kura 8,208 katika kata nane kati ya kata 22 dhidi ya John Palingo ambaye alipata kura 2,295.

Jimbo la Dodoma Mjini Peter Chiwanga alipata kura 3,183, Georvin Malole 2,479 huku Adam Kimbisa akipata kura 214 katika kata 18 kati ya 37.

Wakongwe wengine waliodondoshwa ni mbunge wa Rorya mkoani Mara, Profesa Philemon Sarungi, ambaye ameangushwa na diwani wa Kata ya Koryo, Lamek Airo.

Profesa Sarungi, ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ameangushwa mfanyabiashara maarufu Airo.

Katika orodha hiyo ya wakongwe pia wamo mbunge wa Mufindi mkoani Iringa, Joseph Mungai, ambaye ameangushwa na Mahamudu Mgimwa huku Mbunge wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir, akipigwa kumbo na Said Mtanda.

Mungai aliwahi kuwa Waziri wa Elimu huku Mudhihir akiwa Naibu Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo.

Kimaro adondoshwa Vunjo

Kutoka mkoani Kilimanjaro, Rodrick Makundi anaripoti kuwa, Mbunge wa jimbo la Vunjo, Aloyce Kimaro, amedondoshwa kwenye kura za maoni, ambapo Crispin Meela ameibuka kidedea.

Wanasiasa wengine waliokuwa wakiwania jimbo hilo ni aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, James Kombe.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, Meela ameshinda kwa kura 7,162, Kimaro (3,194) Kombe kura 1,110 na Thomson Moshi (788).

Jimbo la Moshi Mjini, aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiusa, Athuman Ramole, ameibuka mshindi katika mchakato huo akiwashinda wapinzani wenzake tisa.

Ramole amepata kura 1,554, akifuatiwa na Mwenyekiti wa WAZAZI mkoa wa Kilimanjaro, Thomas Ngawaiya (1,539) na Justine Salakana (1,152).

Jimbo la Moshi Vijijini, Mbunge anayemaliza muda wake, Dk. Cyril Chami ameibuka mshindi kwa kura 9,196 dhidi ya mpinzani wake Ansi Mmasi (2,791).

Jimbo la Mwanga, mbunge anayemaliza muda wake Profesa Jumanne Maghembe, ameshinda kwa kura 10,743 huku Joseph Thadayo akipata kura 6,889.

Jimbo la Siha, Naibu Waziri wa TAMISEMI Agrrey Mwanri, ameibuka kidedea baada ya kukosa mpinzani.

Majimbo la Same Mashariki na Magharibi, yanayoshikiliwa na Anne Kilango na Dk. Mathayo David, walikuwa wakiongoza.

00000

Chambiri amng’oa Kwaangw’

Kutoka mkoani Manyara, Tabia Daffo, anaripoti kuwa Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ile Sendeka, ametetea nafasi yake licha ya kukabiliwa na ghasia kubwa.

Ghasia hizo zilizuka baada ya mwanachama mmoja kutoweka na daftari lenye orodha ya wapiga kura wa tawi la Landanai na hivyo uchaguzi huo kurudiwa kwenye kata za Terat, Ruvuremiti, Lobosiret na Naberera.

Katika Jimbo la Babati, mbunge anayetetea nafasi hiyo Omar Kwaangw’, ameangushwa na aliyekuwa Mbunge wa Tarime mkoani Mara, Kisyeri Chambiri.

Katika Jimbo la Babati Vijijini, mambo yamemwendea vibaya mbunge wake wa sasa Damas Nakei, ambapo Mwenyekiti wa Wazazi mkoa Manyara, Jittu Vrajlal Soni, ameibuka mshindi.

Jimbo la Hanang, mbunge wa sasa Dk. Mary Nagu, amefanikiwa kumshinda mpinzani wake wa karibu Rose Kamili, ambaye ni mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa.

Dk. Wanyancha ang’oka

Kutoka mkoani Mara, Samson Chacha na Eva-Sweet Musiba, wanaripoti kuwa Mkuu wa wilaya ya Kwimba, Christopher Kangoye, ameongoza Jimbo la Tarime na kumshinda mpinzani wake wa karibu Nyambari Nyangwine.

Jimbo la Serengeti, matokeo yanaonyesha kuwa mbunge wa sasa Dk. James Wanyancha, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, amepigwa kumbo na Dk. Steven Kebwe.

Jimbo la Musoma Mjini, mbunge anayemaliza muda wake, Vedastus Mathayo, ameibuka mshindi kwa kura 6,489 akifuatiwa na Eliud Tongora aliyepata 3,771.

Kwa upande wa madiwani walioshinda na kata zao kwenye mabano ni Ally Jama (Iringo), Heri Zebedayo (Kitaji), Goldon Mumbala (Nyasho), Madali Kerenge (Mwigobero), Swahib Mohamed (Nyakato), John Matesi (Kamnyonge), Deogratius Ndege (Bweri), Daud Misango (Mwisenge), Patric Gumbo (Makoko), Masumbuko Magesa (Nyamatare ) na John Mawazo (Kamnyonge).

Katika Jimbo la Musoma Vijijini, mbunge anayemaliza muda wake, Nimrod Mkono ameshinda kwa kura 34,113 akifuatiwa na Antony Mtaka aliyepata 5,940.

Mkuchika, Chikawe
Hawa Ghasia kidedea

Kutoka Mtwara Rashid Mussa, anaripoti kuwa mawaziri watatu, Hawa Ghasia (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), George Mkuchika (Habari Utamaduni na Michezo) na Matias Chikawe (Katiba na Sheria), wamefanikiwa kumeibuka kidedea kwenye majimbo yao .

Mkuchika, amefanikiwa kutetea Jimbo la Newala, Hawa ametetea Jimbo la Mtwara Mjini na Chikawe, Nachingwea.

Hata hivyo, wabunge watatu mkoani hapa, Mohamedi Sinani (Mtwara Mjini) na Suleiman Kumchaya (Lulindi) na Raynald Mrope (Masasi), wameangushwa.

Hawa ameongoza kwa kura 17,000 na kumshinda mpinzani wake Said Nyengedi, aliyepata kura 6,000.

Mkuchika ameongoza kwa kura 9,650 dhidi ya Rashid Akbaru, aliyeambulia kura 6,602.

Chikawe ameongoza kwa kura 2820 dhidi ya 1,162 za Bernad Mnalli.

Katika Jimbo la Mtama, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, amepata ushindi wa kishindo baada ya kupita bila kupingwa.

Jimbo la Mtwara Mjini, Sinani ameangushwa na Hasnein Murji.

Dk. Lorri aibuka Karatu

Naye Shaban Mdoe na Lilian Joel, wanaripoti kuwa baadhi ya wabunge wameshindwa kutetea nafasi walizonazo baada ya kudondoshwa.

Katika Jimbo la Arusha Mjini, mbunge anayemaliza muda wake Felix Mrema, ameangushwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA) Dk. Batilda Burian.

Jimbo la Karatu, mgombea Dk. Wilbroad Lorri, ameibuka kidedea kwa kura 82,460 akifuatiwa na Sixbert Kardya 3,078.

Jimbo la Monduli, Edward Lowassa, ameibuka na ushindi mkubwa na kumtupa mbali mpinzani wake Salash Toure. Lowassa ameibuka na kura 38,262 dhidi ya 321 za Toure.

Jimbo la Longido Mike Lekule Laizer ameongoza kwa kura 13,267 katika kata 14 kati ya 16 za jimbo hili.

Mpesya ‘amliza’ Mwang’oda

Naye Innocent Ng’oko kutoka Mbeya anaripoti kuwa wabunge wawili mkoani hapa, wapo kwenye hali mbaya na wanaweza kudondoshwa. Wabunge hao ni Esterina Kilasi (Mbarali) na Dk. Guido Sigonda (Songwe).

Jimbo la Mbeya Mjini, mbunge anayemaliza muda wake Benson Mpesya, ameibuka na ushindi kwa kura 5,586 dhidi ya 3,362 za Thomas Mwang'onda.

Jimbo la Mbeya Vijijini, Mchungaji Luckson Mwanjale, ameibuka na ushindi wa kura 7,353 akifuatiwa na Andrew Saire 1,902.

Jimbo la Kyela, mbunge anayemaliza muda wake Dk. Harrison Mwakyembe, ameibuka kidedea kwa kura 7,658 dhidi ya 574 za George Mwakalinga.

Jimbo la Rungwe Mashariki, Profesa Mark Mwandosya, ameibuka na ushindi wa kura 4,240 dhidi ya 228 za Steven Mwakajumulo.

Katika Jimbo la Ileje mgombea Ariko Kibona, anaongoza kwa kura 5,849 huku Jimbo la Songwe, matokeo yakionyesha Philipo Mulugo kuwa na kura 7,100. Wanaomfuata ni mbunge wa zamani Poul Ntwina kura 1,968 na mbunge anayemaliza muda wake, Dk. Sigonda akipata kura 780.

Jimbo la Lupa, mbunge anayemaliza muda wake Victor Mwambalaswa, ameibuka kidedea kwa kura 6,135 akifuatiwa na mbunge wa zamani, Njelu Kasaka kura 4,135.

Jimbo la Mbarali, Modestus Kilufi anaongoza kwa 1,521 akifuatiwa na Burton Kihaka kura 1,332 huku mbunge anayemaliza muda wake, Esterina Kilasi akiambulia kura 614.

Jimbo la Rungwe Magharibi, mbunge anayemaliza muda wake na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, ameshinda kwa tofauti ya kura 1,000 dhidi ya Richard Kasesera.

------------------------------------------
Kutoka Iringa Anita Boma, anaripoti kuwa wabunge sita wa zamani wameangushwa kwenye kura za maoni huku wapinzani wao wa karibu wakitamba.

Wabunge walioangushwa ni Joseph Mungai (Mufindi Kaskazini), Monica Mbega (Iringa Mjini), Jackson Makweta (Njombe Kaskazini), Profesa Raphael Mwalyosi (Ludewa), Benito Malangalila (Mufindi Kusini) na Yono Kevela (Njombe Magharibi).

Monica Mbega, ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ameangushwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela huku Makweta akiangungwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Deo Sanga na Mungai akiangushwa na Mahamudu Mgimwa

Katika Jimbo la Iringa Mjini Mwakalebela ameongoza kwa kura 3,897 dhidi ya 2,989 za Monica.

Jimbo Mufindi Kusini, mbunge anayemaliza muda wake Benito Malangalila, ameangushwa na Mendradi Kigola.

Jimbo la Kilolo, ndoto za Venance Mwamoto kumng’oa Profesa Msolla, zimeota mbawa baada ya kuangushwa kwa kura 18,000 dhidi ya zake 3,000.

Jimbo la Isimani mbunge anayemaliza muda wake William Lukuvi, ameshinda kwa kura 7,996 dhidi ya kura 533 za Festo Kiswaga, 286 za Leonard Mwali na Yahaya Mtete aliyepata kura 176.

Jimbo la Kalenga, Steven Galinoma ameangushwa na Dk. William Mgimwa, kwa kura 2,819 akifuatiwa na Abas Kandoro aliyepata kura 2,353.

Jimbo la Ludewa Profesa Mwalyosi, ameangushwa na Deo Filikunjombe. Matokeo yanaonyesha Filikunjombe amepata kura 6,000 dhidi ya 4000 za Profesa Mwalyosi.

Jimbo la Njombe Magharibi, mbunge anayemaliza muda wake Yono Kevela ameangushwa na Thomas Nyimbo.

Jimbo la Makete, mbunge anayemaliza muda wake Dk. Benelith Mahenge, atetea nafasi hiyo kwa kuibuka kidedea huku Naibu Spika Anne Makinda, akitetea Jimbo la Njombe Kusini.

No comments:

Post a Comment