Friday, 20 May 2011

DKT. BILAL MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA WAUGUZI MNAZI MMOJA DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisoma hotuba yake wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salam leo Mei 20.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimkabidhi zawadi, Paul King’ara Muuguzi kutoka mkoani Mwanza wakati wa maadhimisho ya Sherehe za ya miaka 40 ya kuzaliwa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salam leo Mei 20.
Catherine Magole, akikabidhiwa zawadi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo ya jinsi wauguzi wanavyofanya kazi kuhusu mishipa ya fahamu na Ubongo, kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania Tawi la Moi, Prisca Tarimo, wakati alipotembelea banda la Moi Dharura, kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salam leo Mei 20.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Muuguzi mstaafu Jito Ramu, aliyekuwa mmoja kati ya wauguzi waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salam leo Mei 20. Dkt Bilal alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Wauguzi waliohudhuria sherehe hizo wakila kiapo mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa sherehe hizo.
Wauguzi wakipita na mabango yenye ujumbe mbalimbali mbele ya mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salam leo Mei 20.
Baadhi ya wauguzi wakiserebuka kushangilia sherehehe hiyo wakati msanii wa muziki Mrisho Mpto, walipokuwa akitoa burudani kwenye sherehe hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Udhamini baada ya sherehe hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wenyeviti wa Mkoa na Wauguzi wakuu wa Hospitali za Mikoa.Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment