Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi mil. 7 kwa Bw. Paul Luvinga alieibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha "Shujaa wa Safari Lager" kilichomalizika usiku huu katika ukumbi wa hoteli ya Paradise,Benjamin Mkapa Tower,Jijini Dar.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Butallah na katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Mahusiano TBL,Steven Killindo.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akimkabidhi Tuzo ya "Shujaa wa Safari Lager" Bw. Paul Luvinga alieibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho usiku huu katika ukumbi wa hoteli ya Paradise,Benjamin Mkapa Tower,Jijini Dar.Katikati anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akitangaza mshindi wa Tuzo za "Shujaa wa Safari Lager" usiku huu.huku Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja (katikati) na Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Butallah wakisikiliza.
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Butallah akizungumzia namna shindano hilo lilivyoendeshwa mpaka kufikia kupatikana tatu bora walioingia katika fainali za Shujaa wa Safari Lager.
Mh. Mahanga akipeana mkono na Bw. Leonard Mtepa ambaye alikuwa ni mmoja kati ya watatu waliofika katika hatua ya tatu bora ya Shujaa wa Safari Lager usiku huu.
Washiriki watatu waliofika katika hatua ya fainali ya shindano la Sujaa wa Safari Lager wakiwa na mifano ya hundi zao zao walizokabidhiwa usiku huu.toka kulia ni Bw. Leonard Mtepa,Mercy Shayo na Paul Luvinga.
Wakurugenzi wa TBL wakiwa katika mazungomzo.kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko,David Minja na kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Mahusiano TBL,Steven Killindo.
Mh. Waziri akiondoka ukumbini hapo hukua akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM,Mh. Beno Malisa (kushoto).
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM,Mh. Beno Malisa (kulia) akiwa na Mdau Victor Lebulu (shoto) pamoja na Mdau wa Kampuni ya Executive Solition.
Washiriki wengine wa wawili waliokupo katika tatu bora ya Shujaa wa Safari Lager,Leonard Mtepa (kushoto) na Mercy Shayo (kulia) wakifuatilia mchakato mzima unavyokwenda.
No comments:
Post a Comment