Tuesday 6 March 2012

Maandalizi kabambe mkoa mpya wa Njombe

Mbunge wa Jimbo la Njombe Kusini na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika kijiji cha Idundilanga.

Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kutangaza nia ya kuugawa mkoa wa Iringa ili kuwa na mikoa miwili yaani mkoa wa Iringa na Mkoa wa Njombe, wananchi wa mkoa mpya wa Njombe hawalali hadi kieleweke. 

Kwa kujituma kunakostahili kuwa mfano wa kuigwa na kwa ushirikiano usiojali imani, kabila au itikadi za kisiasa wamedhamiria kuujenga mkoa wao huo kwa kiwango cha hali ya juu. 

Mbinu wanazotumia ni kupiga vita umaskini kwa kuchapa kazi hususan za kilimo cha mazao ya chakula (mahindi, matunda, viazi,) na biashara (miti ya mbao), kupiga vita ujinga kwa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na shule ya awali na msingi pamoja na kila kata kuwa na shule ya upili, na kupiga vita maradhi kwa kujenga zahanati na vituo vya afya.

 Wakionesha ari na msukumo mkubwa kwa Mbunge wao Mhe. Anne Semamba Makinda aliyewatembelea wananchi hao hivi karibuni, wananchi hao wanajivunia tabia yao ya kupenda kufanya kazi kwa bidii na kujituma, ardhi yenye rutuba walio nayo pamoja na ukanda wanamoishi wa nyanda za juu kusini wenye mvua za kutosha nyakati zote.

Akizungumza nao mbunge huyo aliwasisitizia kujipanga vizuri ili kuzifaidi fursa zitakazotokana na uchimbaji wa mkaa wa mawe pamoja na chuma katika migodi ya Ludewa na Liganga ambayo utekelezaji wake tayari uko katika hatua za kuanza uchimbaji. Zifuatazo ni baadhi ya shughuli ambazo wananchi wa Njombe wanashiriki.






No comments:

Post a Comment