Mmoja wa waamuzi wa mchezo wa ufunguzi wa mpira wa miguu kati ya mabingwa watetezi wa michuano ya Kombe la NSSF, akifanya uhakiki wa wachezaji wa mabingwa hao kabla ya mpambano wao na TBC, kwenye Uwanja wa Sigara, Chang'ombe, Dar es Salaam leo asubuhi. (Picha na Kassim Mbarouk)
Mwamuzi akifanya uhakiki wa wachezaji wa TBC katika mpambano huo wa ufunguzi, ambapo bingwa mtetezi Jambo Leo, iliichapa TBC, mabao 2-1.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano hayo, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, akisalimiana na mwamuzi wa mpambano huo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau. |
Waziri Kabaka, akisalimiana na wachezaji wa Jambo Leo kabla ya mpambano huo.
Waziri Kabaka, akisalimiana na wachezaji wa TBC.
Wachezaji wa TBC, wakisalimiana na wa Jambo Leo kabla ya kupambana katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo. |
Waziri Kabaka, akizungumza na waachezaji katika ufunguzi huo, Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau na wa pili ni Mwenyekiti wa NSSF.
Waziri Kabaka, akipiga mpira katikati ya Uwanja wa Sigara (TCC), Chang'ombe, ili kuyafungua mashindano hayo.
Wachezaji wa akiba wa timu ya Jambo Leo, wakifuatilia mpambano kati ya timu hizo leo asubuhi.
Waziri Kabaka akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau.
Wachezaji wa timu za Netbal za Mwananchi (bluu), wakipambana na wa IPP Media katika ufunguzi huo. IPP iliishinda Mwananchi kwa Points 16-12.
Mchezaji wa IPP Media, akiwatoka waandishi wa Mwananchi katika mpambano wao wa Ufunguzi.
Akina dada wa Zanzibar, wakisalimiana na wenzao wa Global Publisher (kijani), kabla ya kuanza kwa mpambano wao katika ufunguzi huo.
Wachezaji wa Zanzibar, wakiwa na mpira wakijaribu kufunga bao kwenye mchezo huo.
Kundi la Simba Theatre, likitumbuiza katika ufunguzi wa michuanao hiyo.
Wanenguaji wa kundi hilo, wakicheza ngoma za asili za makabila ya Wamakonde wa Kusini. Picha na Bayana Blog
No comments:
Post a Comment