Friday, 30 September 2011

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YAZINDUA WIKI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU

 Baadhi ya maofisa wa Afya wakisikiliza otuba ya kuzindua rasmi wiki ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika kusheherekea miaka 50 ya Uhuru
 Dkt. Deo Mtasiwa akitambulisha meza kuu kwa wageni waalikwa na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kusheherekea miaka 50 ya Uhuru.
 Pichani Juu na Chini ni  baadhi ya Wakurugenzi, Viongozi wa Wizara na Serikali, Wadau wa Sekta ya Afya na Watoa huduma za Afya.
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Rufaro Chatora akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo ameipongeza Tanzania kwa hatua iliyofikia katika kuboresha huduma ya Afya.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Hussein Mponda akitoa hotuba ya kuzindua rasmi wiki ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika kusheherekea miaka 50 ya Uhuru ambapo pamoja na mambo mengine ameelezea vipaumbele vitakavyozingatiwa baada ya miaka 50 ya Uhuru kuwa ni pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma za Afya na Ustawi wa Jamii,  Kuimarisha huduma za Afya ya Wanawake wajawazito, watoto wachanga na watoto wenye umri chini ya miaka 5 ikiwa ni pamoja na kuimarisha udhibiti wa magonjwa yanayoammbikiza na yasiyoambukiza pamoja na yale yaliyosahaulika.Pia ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kupima Bure Afya zao na kipindi chote cha wiki ya maadhimisho hayo itakayomalizika tarehe 2, Oktoba, 2011.
 Mwanamuziki Mkongwe nchini Kassim Mapili (katikati) akiwa na wanamuziki wenzake wa bendi ya Mjomba wakitoa burudani katika sherehe za maadhimisho hayo
 Baadhi ya wageni katika hafla hiyo.

 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Rufaro Chatora(kushoto), Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Margareth Mhando (katikati) na Mkurugenzi wa Bima ya Afya Dkt. Emmanuel Humba wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi.
 Mgeni rasmi Mh Dkt. Mponda akisakata Rhumba baada ya kukunwa na muziki uliokuwa ukiporomoshwa na Mzee Kassim Mapili.
  Mfanyakazi wa Banda la kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele ambayo ni Usubi, Matende na Mabusha, Kichocho na Vikope akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Dkt. Mponda alipotembelea banda hilo. Kulia ni Dkt. Alison Mjema.
 Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Mlandwe Madihi (mwenye miwani) akimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi Dkt.Mponda alipotembelea banda la Taasisi hiyo.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akizungumza na  Jumanne Ramadhani (wa kwanza kushoto) pamoja na wafanyakazi wenzake wa Banda la TAYOA ambapo amewasisitiza kuongeza juhudi katika kutoa elimu kwa vijana juu ya maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi na njia za kujikinga.

No comments:

Post a Comment