Saturday, 26 February 2011

BONGO FLEVA WAITUNGUA BONGO MOVIE BAO 2-0

Mshambuliaji wa timu ya Bongo Freva,Ali Kiba akijaribu kutaka kumtoka beki wa timu ya Bongo Movie katika mtanange wa Kuchangia maafa ya Gongo La Mboto uliomalizika jioni hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar.Bongo Freva iliibuka kidedea kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimyani na mshambuliaji H. Baba katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
Kiungo wa Bongo Movie,Ben Kinyaiya akipiga penati na kukosa kwa kupiga nje.
Mshambuliaji wa kushoto wa timu ya Bongo Freva,KR Mullah akimtoka mchezaji wa timu ya Bongo Movie katika mchezo uliopigwa jioni hii katika uwanja wa Taifa.
Mshambuliaji wa timu ya Bongo Freva,H. Baba akiipachia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Bongo Movie katika mtanange wa kuchangia maafa ya Gongo la Mboto uliopigwa jioni hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar.
Hatari langoni mwa Bongo Movie.
Nyanda wa timu ya Bongo Freva,Tunda Man akionyesha utaalamu wake mbele ya mchezaji wa timu ya Bongo Movie,Joti katika mtanange uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar.
Bongo Freva wakishangilia ushindi waoo.
Vingwanga vilitawala kabla ya mchezo kuanza kwa upande wa wana Bongo Movie.


Mgeni Rasmi katika mchezo huo,Meya wa Ilala,Mh. Jerry Slaa akikagua timu kabla ya mchezo.
Timu ya Bongo Movie.
Timu ya Bongo Freva.
Uwanja ulifurika sana kwa kweli,hii inaonyesha ni kiasi gani watu walivyohamasika katika swala zima la kuchangia wahanga wa mabomu kule Gongo la Mboto.


No comments:

Post a Comment