Thursday, 17 February 2011

Rais Kikwete atembelea kambi ya JWTZ gongo la mboto leo

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na vyombo vya habari pindi alipotembelea katika kambi ya Jeshi la Wananchi ya KJ 511 iliopo huko Gongo la Mboto mara baada ya milipuko ya Mabomu katika kambi hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika kambi ya KJ 511 eneo la Gongo la Mboto wakati alipofika kujionea athari za mlipuko wa mabomu katika kambi hiyo
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.Hussein Mwinyi (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange na Mnadhimu Mkuu wa jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali Abdulrahman Shimbo katika kambi ya KJ 511.Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwafariji baadhi ya watoto waliopotelewa na wazazi wao kutokana na mlipuko wa mabomu.
Wakazi wa Gongo la Mboto wakilazimika kupanda malori kutokana na uhaba wa usafiri katika eneo hilo mara baada ya milipuko ya mabomu.
Moja ya Nyumba zilizodhurika na Milipuko ya Mabomu hayo.
Hivi ndivyo hali ya usafiri ilivyokuwa leo mara baada ya milipuko hiyo.
Mkazi wa Gongo la Mboto, Regina Mlawa akionyesha nyumba yake jinsi ilivyoharibika.
Moja ya Mabomu yaliyokuwa yakiripuka huko Gongo la Mboto usiku wa kuamkia leo linavyoonekana mara baada ya kuripuka.
Sehemu ya majeruhi waliohifadhiwa katika hospital ya Amana,jijini Dar.
Mkazi eneo la Majoe, Mbwana Hassan akiwa na mtoto wake mgongoni, Hamidu Hassan akipita mbele ya kambi ya KJ 511 wakati akijaribu kunusuru maisha yake.
Wengine walipoteza fahamu kwa mshtuko.
usafiri ulikuwa ni wa shida sana katika eneo hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel wakitoa msaada wa maji, vyakula, juice pamoja na magodoro.

No comments:

Post a Comment