Thursday, 17 February 2011

Makamu wa Rais atembelea Kambi ya JWTZ Gongolamboto

Mkuu wa Bohari Kuu ya JWTZ C O 511KJ Kanali Mwanjire, akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal moja ya sehemu zilizoathirika na milipuko ya Mabomu kwenye Ghala la kuhifadhia Silaha katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania Gongolamboto jijini Dar es salaam jana jioni, wakati Makamu wa Rais alipotembelea eneo hilo leo.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni General Abrahamani Shimbo, akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal Mabaki ya Mabomu yaliyoripuka kwenye Ghala la kuhifadhia silaha katika Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania Gongolamboto jijini Dar es salaam, wakati Makamu wa Rais alipotembelea eneo laKambi hiyo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitembelea sehemu ya Ghala la kuhifadhia Silaha iliyoathirika kwa milipuko ya Mabomu jana jioni katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania Gongolamboto jijini Dar es salaam leo. wa pili kulia Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Lt General Abrahamani Shimbo.

No comments:

Post a Comment