Wednesday, 9 February 2011

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA 2011 NI RAHA TUPU

Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara,Yusuf Mahmoud akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Tamasha hilo usiku huu katika viwanja vya Ngome Kongwe,Zanzibar.Makamu Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti Za Busara,Simai Said akitambulisha baadhi ya wadau wakuu walioweza kufanikisha Tamasha hilo kwa mwaka huu wa 2011 katika viwanja vya Ngome Kongwe usiku huu.
Baadhi ya Wadau wa Sauti Za Busara 2011 wakiwa katika picha ya pamoja.
Wadau wa Sauti Za Busara wakiserebuka kwa raha zao na kibao kilichopigwa na Mwanamuziki Samba Mapangala kinachohusiana na Tamasha hilo.Bendi ya Percussion Discussion Africa kutoka nchini Uganda ikitumbuziza usiku huu katika Tamasha la Sauti Za Busara 2011 ndani ya viwanja vya Ngome Kongwe,Visiwani Zanzibar.Kikundi cha Ngoma cha Wanyambukwa kutoka Mkoani Dodoma,Tanzania kikitumbuza moja ya nyimbo zao za asili ya Kigogo.
Mwanamuzi wa Christine Salem akifanya vitu vyake usiku huu katika viwanja vya Ngome Kongwe,Visiwani Zanzibar.
Vijana wanaounda kundi liitwalo Maulidi ya Homu ya Mtendeni wa hapa hapa visiwani Zanzibar,Wakifanya vitu vyao usiku huu.
Vijana wa Jahazi Modern Taarab,wakikirudi Kiduku kwa staili ya aina yake wakati wa muendelezo wa Tamasha la Sauti Za Busara 2011 usiku huu ndani ya viwanja vya Ngome Kongwe,Zanzibar.
Waimbaji wa Bendi ya Jahazi Modern Taarab wakilitawala jukwaa kisawasawa usiku huu wa Tamasha la Sauti Za Busara,Ngome Kongwe.
Mdau Bandago a.k.a Hamis Ma SMS pamoja na mpambe wake wakifarilia Tamasha la Sauti Za Busara Usiku huu.
Wadau.
Ankal Albert Makoye na Ankal Mabrouk.
Wadau.

No comments:

Post a Comment