Saturday, 19 March 2011

MPAMBANO WA MSONDO NA SIKINDE WAFANA SANA

Mwanamuzi Shaban Dede aliejiunga na Msondo Ngoma Band hivi karibuni akiimba moja ya nyimbo zake akizowahi kuziimba enzi hizo akiwa na bendi hiyo kabla ya kuihama.
Shaban Dede wa Msondo Ngoma akifanya kweli katika sindano lao dhidi ya watani wao wa jadi Sikinde katika show iliyofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee holi.
Wataalam wa kupuliza midomo ya Bata wa Msondo Ngoma Band wakiwaburudisha mashabiki wao.
Hussein Jumbe wa Sikinde akiimba nyimbo yake ya Nachecheme aliyoiimba miaka ya nyuma wakatia akiwa na bendi hiyo kabla ya kuihama na kuirudia tena siku za hivi karibuni.
Madansa wa Sikinde Ngoma ya Ukae wakiwaburudisha mashabiki wao usiku wa kuamkia le ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee holi kulikofanyika show ya mashindano kati ya mahasimu wawili,Sikinde na Msondo.
Hata Ankal Othman Michuzi Jr wa http://othmanmichuzi.blogspot.com hakuwa nyuma kwenda na ile staili ya Msondo Ngoma katika show iliyofanyika usiku wa kuamkia leo,Diamond Jubilee holi.
Mkongwe Samba Mapangala a.k.a mzee wa kuvunja mifupa akiwasalia mashabiki wa Msondo na Sikinde waliofurika katika ukumbi wa Diamond Jubilee holi.
Mzee Kitime a.k.a JFK akizisaka taswirazz.
Wazee wamekutana,Kulia ni Mzee Kassim Mapile na Mzee Samba Mapangala.
Hapa kazi ipoooo........
Mzee wa Jiachie ilibidi aweke kando kamera na kuingia katika dimba la dansi kuonyesha umahiri wake.
Mwanadada akimpa tafu ya kulisakata ngoma la Msondo Ngoma.
Mzee Mzima Maalim Muhidin Gurumo akiwa na mai waifu wake wakifatilia mpambao huo.
Dimba limependezaaaa...
Wadau mbali mbali walikuwepo katika mpambano huoo.

No comments:

Post a Comment