Saturday 26 March 2011

tuzo za kili music awards 2011 usiku huu

Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo,Dr. Emmanuel Nchimbi akabidhi tuzo ya heshima iliyopata Shirika la Habari Tanzania (TBC) kwa Bosi Mkuu wa TBC,Joe Lugalabamu.
Mwanamitindo Khadija Mwanamboka (kushoto) pamoja na Producer Pancho Latino (pili kulia) wakimkabidhi tuzo ya Msanii Mpya anaechipukia Linnah ambaye pia alijinyakulia tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kike.
Wachezaji wa Soka nchini,Juma Kasseja (kushoto) na Shadrack Nsajigwa (kulia) wakimkabidhi tuzo Mzee Yussuf ikiwa ni tuzo ya Wimbo Bora wa Taarab.
Mzee Said Mabela wa Msondo Ngoma Band,akitoa shukrani zake kwa wapenzi wa Muziki wa Dansi pamoja na wale woote wanaoufanikisha Muziki wa Dansi nchini mara baada ya kupewa tuzo ya Heshima kwa ukongwe alionao katika Muziki.
Mzee Small Ngamba na Bi. Chau wakidhi tuzo kwa Producer Man Water ambaye alimuwakilisha Msanii wake 20% ambaye alijinyakulia tuzo nyingi kuliko wote.hapa alikuwa akipewa tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka.Barnaba akiifurahia tuzo yake ya Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba.Joe Makini akijinyakulia tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop toka kwa Besta pamoja na Marlow.Msanii Cpwaa akitoa shukrani zake za dhati kwa mashabiki wake walioweza kumpigia kura mpaka kuweza kupata tuzo ya Video Bora ya Muziki ya Mwaka.Mbungu wa Viti Maalum wa CCM,Mh. Vicky Kamata akimkabidhi tuzo ya Wimbo Bora wa R&B msanii Ben Poul.Msanii wa vichekesho toka kundi la Orijinal Comedy,ambaye pia ni Mwanamuziki akitoa shukrani zake kwa mashabiki wake waliomuwezesha kupata tuzo ya Wimbo Bora wa Asili wa Tanzania.Msanii mkongwe wa muziki nchini,Lady Jay Dee akiwa na tuzo zake mbili alizojishindia,moja iliwa ni ya Wimbo Bora wa Afrika Mashariki na nyingine ni Msanii Bora wa Kike.Mkurugenzi Mkuu wa Prime Time,Juhayna Kussaga pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja wakimkabidhi tuzo Mtunzi Bora wa Nyimbo abaye ni 20 % akiwakilishwa na Producer wake Man Water.20 % ndie alieibuka kinara wa kupata tuzo nyingi ambazo ni za Wimbo Bora wa Afro Pop,Msanii Bora wa Kiume,Wimbo Bora wa Mwaka pamoja na Mwimbaji Bora wa Kiume.
Tuzo ya Rapa Bora wa Bendi ilienda kwa Khalid Chokoraa kama anavyoonekana hapa akiwa na Josee Mara pamoja na Kalala Junior wanaounda kundi la Mapacha watatu ambapo Bendi yao pia iliweza kupata tuzo ya Wimbo Bora wa Kiswahili.
Tuzo ya Wimbo Bora wa Reggae ilienda kwa Hardmad.
Msanii JCB alijinyakulia tuzo ya Wimbo Bora wa Hip Hop na hapa akitoa shukrani kwa mashabiki wake.
Antonio Nugaz,Ruben Ndege pamoja na Dataz.
Hii ilikuwa ni shoo moja matata sana ambayo haikutegemewa na mtu yeyote,Kati yupo Banana Zorro,Kulia Diamond na kushoto ni Ali Kiba ambao waliimba wimbo wa Tunatoana Roho ulioimbwa na Bendi ya Msondo Ngoma.
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo,Dr. Emmanuel Nchimbi akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa BASATA,Ghonche Mategero wakifatilia kwa makini shughuli nzima ya utoaji Tuzo.
Wadau,toka kulia ni Bosco Majaliwa,Baraka Msilwa,Albert Makoye pamoja na Omary Baraka.
Rais wa RBP,Mama Rahma Al Kharous pia alikuwepo kushuhudia tuzo hizo zikitolewa.
Wadau.
Vijana wa THT wakionyesha mambo yao.

No comments:

Post a Comment