Sunday 5 February 2012

Mh. Kinana aongoza maandamano ya kuadhimisha miaka 35 ya CCM jijini Dar

 Mjumbe wa NEC wa CCM,Mh. Abdulrahman Kinana (katikati),Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick (wa pili kulia) wakiwa pamoja na viongozi mbali mbali wa CCM mkoa wa Dar es Salaam wakishiriki Matembezi maalum ya maadhimisho ya Miaka 35 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ambayo kilele chake kimefanyika jijini Mwanza na Rais Jakaya Kikwete ndie alikuwa mgeni rasmi.
 Matembezi yakiendelea katika barabara ya Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick akihutubia mkutano wa hadhara wakati wa maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick akipeana mkono na Mjumbe wa NEC wa CCM,Mh. Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake leo kwenye viwanja vya Buguruni jijini Dar.
 Mjumbe wa NEC wa CCM,Mh. Abdulrahman Kinana akipigiana saluti na mmoja wa chipukizi waliokuwepo uwanjani hapo.
 Mjumbe wa NEC wa CCM,Mh. Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa jijini la Dar es Salaam mapema leo kwenye uwanja wa Buguruni wakati wa maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM ambayo kilele chake kimefanyika jijini Mwanza na Rais Jakaya Kikwete ndie aliekuwa mgeni rasmi.
 Mjumbe wa NEC wa CCM,Mh. Abdulrahman Kinana (kushoto) akiwa na wanachama wenzake wa CCM.
 Mabango kabla ya kuanza kwa maandamano.
 Sehemu ya Wanachama na Wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa kwenye mkutano huo. 
 Wanamuziki wa Bendi ya Mashujaa wakifanya vitu vyao. 
 Baadhi ya wanachama wa CCM wakiuliza maswali.
 Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Mh. Idd Azzan akizungumza na wananchi wa jimbo lake.
 Diwani wa Hananasifu,Mh. Abbas Tarimba akizungumza kwenye mkutano huo.

No comments:

Post a Comment