Wednesday, 22 June 2011

M-net Afrika yazindua chaneli mpya ya kiswahili jijini dar

Mkurugenzi Mtendaji wa M-Net Afrika Biola Arabi akizungumza jioni ya leo wakati wa uzinduzi wa chaneli mpya ya Kiswahili (AFRICAMAGIC SWAHILI)ndani ya hoteli ya Movenpick jijini Dar,Chaneli hiyo inatarajiwa kuruka hewani Julai 1, 2011.Aidha chaneli hiyo itakuwa ikionekana kwenye nchi  rafiki zinazoongea lugha ya Kiswahili ikiwemo Kenya,Uganda,Rwanda,Ethiopia,Burundi,Congo pamoja na DRC.


Meneja mahusiano  wa Multchoice Tanzania,Barbara Kambongi akiwakaribisha wageni waalikwa,waigizaji wa filamu pamoja na waandishi wa habari kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa chaneli mpya ndani ya DSTV jioni ya leo,jijini Dar.Chaneli hiyo inatarajiwa kurushwa hewani  juni,1,2011
 Mkurugenzi Mtendaji wa COSOTA, Yustus Mkinga akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na waigizaji mahiri wa filamu hapa nchini,kuhusiana na suala la hakimiliki za wasanii,wakati wa uzinduzi wa chaneli hiyo mpya.
 Mmoja wa wacheza  na waandaazi mahiri wa Filamu hapa nchini na wenye kuonesha mafanikio makubwa katika tasnia hiyo,Steven Kanumba akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa chaneli hiyo mpya ya AFRICAMAGIC SWAHILI kupitia DSTV kwenye hoteli ya Movenpick,jijini Dar.
Mmoja waigizaji mahiri hapa nchini,na mtangazaji wa Redio Uhuru,Natasha akifafanua jambo na pia kutaka kufahamu baadhi ya mambo kuhusiana na ushiriki wa wasanii wa hapa nyumbani kupitia chaneli hiyo mpya,ambayo wanaamini wao kama wasanii itasaidi kwa kiasi kikubwa kuzitangaza kazi zao Kitaifa na Kimataifa.
 Pichani kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa M-Net Afrika Biola Arabi,Muwakilishi wa M-Net  Afrika Mashariki Wangeci Murage pamoja na Meneja Masoko wa Multchoice,Furaha Samalu wakiwa mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo na Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa chaneli mpya ya AFRICAMAGIC SWAHILI ndani ya DSTV. Chaneli hiyo itaanza kuonekana kwa baadhi ya nchi ambazo zinazungumza lugha ya Kiswahili ikiwemo Tanzania,Kenya,Ugand,Rwanda,Ethiopia,Burundi,Congo na DRC.

Mmoja wa waongozaji wa filamu hapa nchini kutoka kampuni ya Game Ist Quality,Bwa.Mtitu akitaka ufafanuzi wa baadhi ya mambo kuhusiana na uzinduzi wa hiyo chaneli mpya itakayoanza kurushwa Julai, 1, 2011 ndani ya DSTV.
Baadhi ya mambo yatakayokuwemo ndani ya chaneli hiyo.

 Pichani wa pili kulia ni Meneja huduma wa Multchoice  Ronald Shelukindo akiwa na wadau wengine wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa chaneli mpya ndani ya DSTV itwayo AFRICAMAGIC SWAHILI

 Pichani kushoto ni mmoja wa waigizaji mahiri wa filamu hapa chini Ray pamoja na waigizaji wengine wakiwemo na wadau mbalimbali wakilifuatilia kwa makini tukio hilo adhimu hoteli ya Movenpick jijini Dar.
Wadau mbalili wakishuhudia tukio hilo jioni ya leo.

Pichani kati ni mmoja wa waigizaji mahiri katika mpango mzima wa Stand Up Comedy hapa Bongo,Evansi Bukuku akiwa na wadau wengine wakifuatilia kwa makini yalikuwa yakijiri jioni ya leo wakati wa uzinduzi wa programu mpya ya kiswahili itakayoitwa AFRICAMAGIC SWAHIL ndani ya DSTV.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa ndani ya moja ya ukumbi wa hoteli ya Movenpick jioni ya leo,wakati wa uzinduzi wa programu mpya ya kiswahili itakayoitwa AFRICAMAGIC SWAHIL ndani ya DSTV.

Wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wasanii wa filamu hapa nchini wakiwa ndani ya moja ya ukumbi wa hoteli ya Movenpick jioni ya leo,wakati wa uzinduzi wa programu mpya ya kiswahili itakayoitwa AFRICAMAGIC SWAHIL ndani ya DSTV,

No comments:

Post a Comment