Friday 24 June 2011

MICHORO YA RAZA MOHAMMED NA MWANAE EDDY YASTAWISHA JINA LA TANZANIA LONDON


Mzee Raza akila pozi na Mwanae Eddy Katika baadhi ya kazi zake.

Salam,

Utamaduni na sanaa ya Mtanzania vimewasisimua watazamaji waliohudhuria maonyesho ya mchoraji Raza Mohammed mjini London siku chache zilizopita. Mzee Raza Ameanza kazi ya Kuchora picha tokea kipindi cha uhuru mojawapo ya kazi zake ni pamoja na "TINGATINGA", JUMA NA ROZA. Pia amewahi kuwachora Baadhi ya Viongozi wetu kuanzia Rais Mstaafu Mwinyi na Jakaya kikwete n.k

Akifungua maonyesho hayo yatakayoendelea kwa mwezi mzima kwa niaba ya serikali, Kaimu Balozi wa Tanzania Uingereza, Mheshimiwa Chibaka Kilumanga alilishukuru shirika la Global Fusion Music and Arts (GFMA) chini ya uongozi wa Louisa Le Marchand kusaidia kutayarisha shughuli hii.

Bwana Kilumanga alisema Raza alialikwa Uingereza awali kusaidia sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Bongo.
Mh Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Chabaka Kilumanga akiwa kwenye picha ya pamoja na Mzee Raza, Eddy, Freddy Macha na wadau wengine.
mdau akimwuliza Mzee Raza maswali kuhusiana na kazi yake.
kutoka kushoto Freddy Macha akifurahia Jambo na Baraka Baraka wakiwa na wadau wengine.
wadau wakipata vinywaji na vitafunio.
wadau wakijadiliana.
wadau mbalimbali walijitokeza kuangalia kazi za Mzee Raza na Mwanae Eddy.
Freddy Macha akiwa kazini na bendi Ya Global Fusion wakiwatumbuiza wadau waliojitokeza kuja kwenye onyesho la Picha.
Eddy(Kulia) akitoa maelekezo kwa babake .
Eddy mwenye kofia akiwa na Babake Mzee Raza wakiweka picha ukutani.
Eddy mwenye kofia akiwa na Babake Mzee Raza wakiweka picha ukutani.
Baaadhi ya kazi za Eddy.
Picha za Mzee Raza.

No comments:

Post a Comment