Thursday 23 June 2011

TANZANIA YAPATA TUZO YA UN KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA JAMII

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya kufunga maadhimisho ya siku ya Utumishi ya Umoja wa Mataifa na Afrika, ikiwa ni mara ya kwanza kwa hafla hiyo kuadhimishwa Barani Afrika na kufanyika nchini Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, Tuzo ya UN ya mshindi wa pili ya Tanzania katika kutoa huduma bora kwa Jamii (Mkurabita) , wakati Makamu alipofika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Juni 23, 2011 kufunga maadhimisho ya siku ya Utumishi ya Umoja wa Mataifa na Afrika, ikiwa ni mara ya kwanza kwa hafla hiyo kuadhimishwa Barani Afrika na kufanyika nchini Tanzania.
Wafanyakazi wa Ubalozi wa Afrika ya Kusini nchini, wakifurahia tuzo yao baada ya kukabidhiwa.
Balozi wa canada nchini, akipokea tuzo kwa niaba ya nchi yake.
zoezi la kukabidhi tuzo linaendelea kwa wawakilishi wa nchi mbalimbali.
Wawakilishi kutoka Korea, wakipokea tuzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi kutoka nchi mbalimbali waliopata tuzo.
Walipata tuzo hawa ni kutoka Ubalozi wa Afrika ya Kusini, wakifurahia tuzo yao kwa pamoja baada ya kukabidhiwa.
Baadhi ya watu kutoka mataifa mbalimbali walioshiriki wakati wa hafla hiyo ya kutoa tuzo na kufunga maadhimisho hayo katika Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam leo.Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment