Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Manchester United ya nchini Uingereza,Andy Cole (katikati) akiongozana na baadhi ya Wakuu wa Kampuni ya Simu ya Airtel wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa J.K. Nyerere,mapema leo asubuhi.Andy Cole amewasili nchini leo kwa ajili ya kuhamasisha michezo mashuleli kupitia kampeni inayoendeshwa na Kampuni ya Airtel ifahamikayo kwa jina la "AIRTEL RISING STAR".
Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Manchester United ya nchini Uingereza,Andy Cole (pili kulia) akiwa na Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dk. Fenella Mukangara (kushoto),Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania,Sam Elangallor (kulia) pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makongo,Meja Celestin Mwangasi wakionyesha Jezi na Mipira itakayotumika katika katika mashindano ya AIRTEL RISING STAR yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni hapa nchini katika mashule mbalimbali.
Andy Cole (kulia) akiwa katika Mazungumzo na Balozi wa Kenya Nchini,Mh. Mutinda Mutiso (katikati) pindi walipokutana katika chumba cha kusafiria watu maalum (V.I.P Lounge) katika uwanja wa Ndege wa J.K. Nyerere mapema leo asubuhi.kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya.
Andy Cole akisaini moja ya picha zake.
Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dk. Fenella Mukangara (kulia) akiagana na Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Manchester United ya nchini Uingereza,Andy Cole katika viwanja vya Makongo,mara baada ya kutoa somo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Makongo wanaojifunza kucheza mpira wa miguu.katikati ni Katibu Mkuu wa TFF,Angetile Oseah.
Andy Cole akiongozana na Baadhi ya wachezaji wa timu ya Shule ya Sekondari ya Makongo kuelekea katika viwanja vya shule hiyo kwa ajili ya kuwapa somo la mchezo wa mpira wa miguu.
Muwakilishi wa Timu ya Manchester United,Nick Humphrey (pili kulia) akitoa somo kwa wazezaji wa timu ya shule ya Makongo kabla ya kuanza kupewa somo na Andy Cole (kulia) mapema leo asubuhi.
Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dk. Fenella Mukangara akitangaza kuzinduliwa rasmi kwa mashindano ya AIRTEL RISING STAR kwa shule za sekondari nchini.uzinduzi huo umefanyika leo katika shule ya Sekondari ya Makongo jijini Dar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania,Sam Elangallor akizungumza katika uzinduzi huo uliojumuishwa na ujio wa Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Manchester United ya nchini Uingereza na Balozi wa timu hiyo,Andy Cole.
Andy Cole akitoa somo.
Andy Cole akionyesha umahiri wake katika kulisakata kabumbu alipokuwa akitoa somo kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Makongo ya jijini Dar mapema leo asubuhi.
Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dk. Fenella Mukangara akiteta jambo na Katibu Mkuu wa TFF,Angetile Oseah.
Andy Cole akitoa somo kwa Nyanda wa timu ya Sekondari ya Makongo leo.
Nyanda wa Shule ya Makongo akirukia mpira bila mafanikio wakati wa mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Manchester United ya nchini Uingereza,Andy Cole katika viwanja vya shule hiyo mapema leo asubuhi.
Ankal Othman Michuzi wa Globu ya Jamii akishoo lavu na Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Manchester United ya nchini Uingereza,Andy Cole.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya. akiteta jambo na Andy Cole.
Andy Cole akimwaga wino katika fulanazz ya Mdau Richard Ngaiza wa Airtel.
Andy Cole akiendelea kumwaga wino wa wadau na wanafunzi wa shule ya Makongo.
Wakitoka katika viwanja vya Makongo mchana huu.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Airtel.
Andy Cole katika picha ya pamoja na Timu ya Shule ya Makongo.
No comments:
Post a Comment