Monday 27 June 2011

TUSHIKAMANE PAMOJA FOUNDATION imetembelea wazee wanao ishi katika mazingira magumu na kutoa misaada mbali mbali.

Kigogo:- Mzee Abdallah Nguzo akilipiwa fedha za mwezi mmoja, kwa mama lishe
ili apate angalau mlo mmoja kwa siku.. Mzee Nguzo hana familia.

Magomeni: Mzee Simba Maduwilo kwa sasa mlemavu wa miguu, na mkewe hali yake ya  afya sio nzuri. wanaishi kwa kumtegemea binti yao anaejishughulisha na mama lishe.
Tandika Kilalakala
wakina mama waliokusanyika sehemu moja kupata misaaada. wengi wao wana ulemavu wa kutembea, hawana kipato na mmoja ana wajukuu wawili walioachwa na wazazi wao.


Vijana wanao ishi na bibi yao, wanapokea nguo na vitabu.


Bibi Mariam Jenga, ana ulemavu wa macho na kutembea kwa shida. Hali ngumu, anawatoto wawili wakike hawana kazi.

Bw. Mohamed, mzee anaesumbuliwa na ugonjwa wa usongo wa mawazo, mkewe kapooza wanatunzwa na mtoto mmoja wa kike hana kazi maalum. hapo amelala anauguza jaraha alianguka na kuungua upande wa mngogo.

Binti wa Mzee Mohamed akitoa maelezo na kusaini misaada aliyopokea


Mbagala: Bi Saada Mohamed, mwenye watot wawili wakike, mmmoja mlemavu wa viungo na mmoja anamatatizo ya afya alipata kupooza.
Wamepata misaada pamoja na mtaji wa gunia la sabuni yakufunga na kuuza rejareja.



Naima Ally ni mama mdogo wa wasichana wa nne waliofiwa na wazazi wote wawili. wamepewa chakula, nguo na vitabu.

Bi Naima akitaisini vitu alivyo pokea.



No comments:

Post a Comment