Friday 17 June 2011

Wafanyakazi wa Airtel wajitolea kuchangia Damu

 Daktari kutoka Huduma ya Taifa ya Damu Salama akichukua damu kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania,Lene Brown ikiwa ni sehemu ya kujitolea katika kuchangia damu salama kwa watoto wanaosumbuliwa na saratani katika Hospitali ya Muhimbili na Ocean Road kama moja ya mchango wake kwa jamii
Madaktari kutoka Huduma ya Taifa ya Damu Salama wakichukua damu kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania,Lene Brown (kushoto) na Frank Makoba waliojitokeza leo kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kujitolea katika kuchangia damu salama kwa watoto wanaosumbuliwa na saratani katika Hospitali ya Muhimbili na Ocean Road kama moja ya mchango wake kwa jamii.Shughuli hii imefanyika mapema leo asubuhi katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliopo Kinondoni Morocco,jijini Dar.
Daktari kutoka Huduma ya Taifa ya Damu Salama,Judith Charle akimpima presha bw. Mkama Manyama wa Kampuni ya simu ya Airtel kabla ya kuanza kwa utaratibu wa kutolewa damu.
Daktari kutoka Huduma ya Taifa ya Damu Salama,Diocles Kaimukilwa akiangalia namna anavyoweza kupata mishipa ili aweze kutoa damu kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania,Clara Mramba mapema leo asubuhi katika makao makuu ya kampuni hiyo.
Utaratibu wa Kujiandikisha ili kuweza kuchangia damu salama kwa ajili ya watoto wanaosumbuliwa na saratani katika Hospitali ya Muhimbili na Ocean Road kama moja ya mchango wa kampuni ya Airtel kwa jamii.Shughuli hii imefanyika mapema leo asubuhi katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliopo Kinondoni Morocco,jijini Dar.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Airtel Tanzania, yenye mtandao mpana na unaotoa huduma nafuu nchini wamejitolea katika kuchangia damu salama kwa watoto wanaosumbuliwa na saratani kama moja ya mchango wake kwa jamii.

Akizungumzia mchango huo, Mkurugenzi wa Utumishi, Perece Kirigiti alisema kuwa kampuni inatambua mchango wake kwa jamii na kwa sasa imeamua kuwashirikisha wafanyakazi wake katika kuchangia damu salama kwa watoto wanaosumbuliwa na saratani katika hospitali ya muhimbili na ocean road jijini Dar es salaam.

“Tutakuwa na zoezi hili siku nzima ya Ijumaa wiki hii katika ofisi zetu makao makuu ya Airtel ambapo wataalamu wa utoaji damu wapatao sita watasaidia zoezi hili lakutoa damu kwa wafanyakazi wa Airtel na watu wengine watakaopenda kushiriki, kwa ajiri yakuwasaidia watoto katika hospitali ya Muhimbili na Ocean road” Alisema

Pia aliongeza kusema, “Weng kati ya wafanyakazi wetu wanafarijika sana kuona mchango wao unasaidia maisha ya watoto Tanzania. Binafsi naunga mkono jitihada hizi na wote tunashiriki katika kujali maisha ya wananchi kwa kuwaunga katika jitihada kama hii na litakua ni jukumu letu katika jamii.”

Akizungumzia zoezi hili, Tunu Kavishe, Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, amesema “ Kwa zoezi hili, wafanyakazi na wadau wetu wanatambua jukumu letu kwa jamii. Na kahuli mbiu yetu mwaka huu ikiwa ni Okoa Maisha”.

Zoezi zima la uutoaji damu kwa mtu mmoja linachukua si zaidi ya dakika 30. Linausisha ujazaji fomu, Usiri wa ushauri na mchangiaji na huwangalizi mzima wa afya ya mchangiaji. Kitendo cha kutolewa damu ni dakika 10 na ni mililita 450 tu kinachoweza kusaidia maisha ya zaidi ya mtu mmoja.

Katika hotuba yake siku ya maadhimisho ya uchangiaji damu duniani mwaka huu,Waziri wa Afya, Dr Hadji Mponda hivi karibuni alisema kuwa ukusanywaji wa damu salama umepanda juu kutoka chupa 52,000 mwaka 2005 hadi kufikia chupa 160,000 mwaka jana,na lengo ni kufikisha chupa 180,000 mwaka huu.

Katika ngazi ya Taifa, jumla ya mahitaji ya damu ni chupa 350,000 hadi chupa 400,000 kwa mwaka ampapo bado inahashiria upungufu mkubwa na kusababisha watu wengi kuwa katika hatari ya kupoteza maisha kutokana na upungufu huo.

No comments:

Post a Comment