Friday, 15 April 2011

Uzinduzi wa Johnny Walker Dodoma hotel

waheshimiwa mbalimbali wakionja ladha murua kabisa ya kinywaji kikali cha Johnny Walker,kama waonekanavyo pichani,kutoka kushoto ni Mbunge wa Afrika Mashariki Mh.Abdalla Mwinyi , Albert Ntabaliba Mbunge wa Manyovu, Nassir Yusuf Korogwe, January Makamba Mbunge wa Bumbuli, Mkurugenzi wa mawasiliano Serengeti Teddy Mapunda, Zitto Kabwe Kigoma Kaskazini, Leticia Nyerere viti maalum Mwanza na mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Caroline Ndungu.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Caroline Ndungu akizungumza nawageni waalikwa mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa vinywaji vikali vya kampuni ya Serengeti Johnny Walker, watu wengi wamehudhuria katika hafla hiyo wakiwemo waheshimiwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyofanyika kwenye moja ya kumbi za mikutano ya Dodoma hotel usiku huu.
Waheshimiwa wakiwa kwenye mazungumzo ya hapa na pale mara baada ya uzinduzi wa kinywaji hicho cha Jonny Walker.
Mmoja wa mabalozi wa kinywjai cha Johnny Walker, Gerald Hando akitoa ufafanuzi wa ladha mbalimbali za kinywjai hicho kwa wageni waalikwa usiku huu.
Balozi mwingine wa kinywaji cha Jonny Walker hapa nchini, Dennis Ssebbo akimimina kinywaji cha Johnny Walker kwa ajili ya kuwapa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliofana sana usiku huu ndani ya hoteli ya New Dodoma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Serengeti (SBL) Teddy Mapunda,akifafanua jambo mbele ya baadhi ya Wabunge waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kinywaji kikali cha Johnny Walker usiku huu,anaefuatia ni Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe, Leticia Nyerere viti maalum Mwanza, Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Caroline Ndungu pamoja na Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini,Mh Peter Serukamba.

Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini ,Mh Zitto Kabwe akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini , Mh Peter Serukamba,Huku Mbunge wa viti Maalum jijini Mwanza,Leticia Nyerere pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL wakishuhudia tukio hilo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL,Teddy Mapunda akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Mh.Peter Serukamba,wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kinywaji kikali cha Johnny Walker mjini Dodoma usiku huu.
Mmoja wa mabalozi wa kinywaji cha Johnny Walker akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa usiku huu kwenye hafla ya uzinduzi wa kinywaji kikali cha Johnny Walker kwa waheshimiwa wabunge pamoja na wageni waalikwa mbalimbali.
Balozi wa kinywaji cha Johnny Walker,Gerald Hando akiwakaribisha wageni waalikwa usiku huu kwnye hafla ya uzinduzi wa tatu wa kinywaji kikali cha Johnny Walker ndani ya New Dodoma hotel usiku huu,aidha katika hafla hiyo wageni waalikwa mbalimbali walihidhuria.
Waheshimiwa wakifurahia jambo,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL,Teddy Mapunda
Katibu Itikadi na Mwenezi wa CCM taifa Nape Nnauye akiingia ukumbini huku akisalimiana na wadau mbalimbali wakati alipohudhuria hafla ya uzinduzi wa kinywaji kikali cha Johnny Walker kutoka kampuni ya bia ya Serengeti iliyofanyika usiku huu kwenye hoteli ya New Dodoma.

No comments:

Post a Comment