Saturday, 30 April 2011

VODACOM MISS TZ YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR

Hivi ndivyo nembo ya Vodacom Miss Tanzania 2011 itakavyokuwa,ilizinduliwa rasmi hapo jana katika Hotel ya kimataifa ya Kilimanjaro Kempnsiky jijini Dares Salaam.
Mkurugenzi wa Lino Internation Agency waandaji wa Miss Tanzania,Hashimu Lundenga akiongea na kuwatambulisha baadhi ya warembo waliowahi kushiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania miaka ya nyuma katika uzinduzi rasmi wa Vodacom Miss Tanzania 2011.
Mkuu wa udhamini wa Vodacom Tanzania,George Rwehumbiza akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya itakayotumika katika shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 na shindano hilo kuzinduliwa rasmi hapo jana katika Hotel ya kimataifa ya Kilimanjaro Kempnsiky wengine ni baadhi ya warembo waliowahi kushiriki katika kinyang’anyiro cha Vodacom miss Tanzania miaka iliyopita.
Mkurugenzi wa Miss Tanzania,Hashimu Lundenga akipiga makofi kwa furaha mara baaada ya nembo mpya ya Vodacom miss Tanzania kuzinduliwa rasmi na mashindano hayo pia.
Mkuu wa udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza akiwasalimu baadhi ya warembo waliowahi kushiriki kinyang’anyiro cha Vodacom miss Tanzania miaka iliyopita ,katika uzinduzi rasmi wa Vodacom Miss Tanzania 2011 uliofanyioka hapo jana katika Hotel ya Kilimanjaro Kempnsiiky.
Baadhi ya viongozi wa kamati ya Vodacom Miss Tanzania pamoja na wadhamini wakuu wa shindano hilo na warembo waliowahi kushiriki shindano la Vodacom miss Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Baadhi ya vimwana waliowahi kushiriki shindano la Vodacom miss Tanzania 2010 ambapo Genevieve Emmanuel (kushoto) ndiye alinyakuwa taji la Vodacom Miss Tanzania 2010 nao walikwepo katika uzinduzi huo.
Mwandaaji wa Miss Chang’ombe Tom mwana wa Chilala katikati akiwa na warembo wake waliowahi kushiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania akiwepo Vodacom miss Tanzania Genevieve Emmanuel (kulia).
Toka kulia ni Meneja udhamini wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa,Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashimu Lundenga,Jokate Mwegelo,Mwandishi wa habari wa The Citizen,Matuto Omary na Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania,Albert Makoye.
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi huo

No comments:

Post a Comment