Tuesday, 6 December 2011

CCM UK YASHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU

Ndugu Maina Owino (M/Kiti CCM UK) akiwahutubia wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua sherehe hizo. Kushoto ni Suleiman Nyerere (M/Kiti Jumuiya ya Watanzania Northampton na katikati ni Mhe. Martha Mlata (Mbunge viti maalum CCM).
mgeni rasmi Mhe. Martha Mlata akiwahutubia wageni waalikwa.
mgeni rasmi Mheshimiwa Martha Mlata (Mbunge viti maalum CCM) akisikiliza hotuba ikitolewa na ndugu Katega (Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM UK), wengine kutoka kushoto ni Leybab Mdegela (Katibu CCM Northampton) Kasongo Mohamed (Kassmoddy) Mjumbe Northampton, Suleiman Nyerere (Mwenyekiti Jumuiya ya Watanzania Northampton) Mgeni rasmi na anayefuata ni Ndugu Maina Owino (M/Kiti CCM UK).
viongozi wa CCM UK, kutoka kushoto Daudi Mwakimwagile (M/Kiti CCM Manchester), Kangoma Kapinga (M/Kiti CCM Southampton) na mwenye kijani na koti jeusi ni Dada Barongo (Katibu CCM Birmngham)
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria sherehe hizo.
Baadhi ya viongozi wa CCM UK wakiwa na mgeni rasmi Mhe. Martha Mlata (Mbunge viti maalumu CCM).
Wageni waalikwa wakipata mlo wwa jioni katika sherehe hizo.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa ccm uk na wageni waalikwa.
Viongozi wa CCM UK wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, kutoka kushoto Hussein Chang’s (Katibu CCM Reading) Peter Gabagambi (M/kiti CCM Birmingham) Barongo (Katibu CCM Birmingham), Mhe. Martha Mlata (Mbunge viti maalum CCM), Kangoma Kapinga (M/Kiti CCM Southampton)
Sehemu ya wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali amabo wana mapenzi nan chi yetu Tanzania nao walijumuika.
Katika picha ni mgeni rasmi Mhe. Martha Mlata na wageni waalikwa wa asili ya Jamiaca ambao walipendezesha sana sherehe hizo kwa kuimba nyimbo ya Taifa la Tanzania kwa Kiswahili.
Kiongozi wa Jamii ya Kijamaica akitoa nasaha zake kuhusiana na harakati za kupigania uhuru ambapo alimsifu sana hayati Muamar Ghadaf kwa ushupavu wake katika kulipigania bara la afrika.
Sehemu ya umati wa watu walihudhuria sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment