Tuesday, 6 December 2011

mkutano wa Kimataifa wa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii ya Ukanda wa Afrika waendelea kwa siku ya pili leo jijini Arusha

 Mwenyekiti wa Kikao kilichouwa kikijadili wajibu wa taasisi za kijamii katika usalama wa watu wanaoishi katika katika mazingira magumu barani Afrika,Bw. Eliud Sanga (Tanzania) (kulia) akiongea wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii ya Ukanda ya Afrika unaondelea leo ilikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.Wengine pichani ni Wajumbe wa Kikao hicho toka kushoto ni Bw. Hafed Choukri (Algeria),Bw. Ephraim Letebele (Botswana),Bw. Frank Odoom (Ghana),Bw. Nathaniel Wellington (Sierra Leone) pamoja na Bi. Brigitte Anguile-mba (Gabon).
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,Dr. Ramadhan Dau pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA,Bi. Irene Isaka wakifurahi jambo wakati Mkutano wa Kimataifa wa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii ya Ukanda ya Afrika unaoendelea leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia kwa makini.
Mtoa Mada wa Kikao hicho,Bw. Nathaniel Wellington (Sierra Leone) akiisoma wakati kwa mkutano huo.

Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii ya Ukanda ya Afrika wakisikiliza kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa leo.








No comments:

Post a Comment