Monday 19 December 2011

TBL yapata Tuzo ya Rais ya Mwaka 2011 ya Mzalishaji Bora

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda akizungumza katika hafla ya utoaji Tuzo za Rais za Mwaka 2011 za Mzalishaji Bora kwa wanachama wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI). Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi kombe Mkurugenzi wa Mahusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steven Kilindo wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais za Mwaka 2011 za Mzalishaji Bora kwa wanachama wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI). Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CTI, Felix Mosha akizungumza katika hafla hiyo.
Vikombe vilivyotolewa kwa washindi.
Mwenyekiti wa CTI, Felix Mosha akipeana mkono na Meneja Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi.
Meneja Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (shoto) akiwa na Meneja wa Mambo ya Nje wa kampuni hiyo, Emma Oriyo huku wakiwa na kombe lao.
Maofisa wa kampuni ya Bia Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja baada ya kukabidhiwa kombe baada ya kushinda Tuzo za Rais za Mwaka 2011 za Mzalishaji Bora kwa wanachama wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI). Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Washindi wa Tuzo za Rais za Mwaka 2011 za Mzalishaji Bora kwa wanachama wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI) wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda wakati wa hafla utoaji wa Tuzo za Mzalishaji Bora kwa wanachama wa CTI.

No comments:

Post a Comment