Hii ndio hali halisi kwa wakazi wa eneo la Jangwani leo mara baada ya mvua kubwa kuendelea kunyesha jijini Dar es Salaam leo na kuyafanya makazi ya wakazi wa eneo hili kuwa namna hii kama zinavyoonyesha picha hizi.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo akijaribu kupita kwenye maji hayo ili afike barabari kwa kujiokoa na mafuriko hayo.
Nyumba zote zimezungukwa na maji huku mengine yakiwa yamejaa ndani ya nyumba hizo.
Kwaambaali anaonekana mmoja wa wakazi wa eneo hilo akiwa kapanda juu ya paa la nyumba yake ili kujirusuru na mafuriko hayo ambayo yameenea katika kila kona ya eneo hilo la Jangwani leo.
Mmoja wa wakazi wa eneo la Jangwani Jijini Dar akiwa amekaa juu ya godoro mara baada ya kuokolewa na waokoaji waliofika katika eneo hilo leo.
Yaani ni kama bahari ilikuwa imeamia hapa maana maji yalienea kila kona.
Askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia wakijaribu kuwazua watu waliokuwa wakiitumia barabara ya morogoro rodi kutokana na kujaa maji kwa barabara hiyo leo.
Wakazi wa Jangwani wakiwa juu ya mapaa yao wakisubiri kupatiwa msaada.
Askari wa Jeshi la Wananchi wakiwa na mtumbwi wakisaidia kuwaokoa wananchi ambao wamekubwa na Mafuriko hayo katika eneo la Jangwani jijini Dar.
Yaani hali ni mbaya sana kwa wakazi wa eneo hili maana mambo ni kama yanavyoonekana pichani hapa.
Helkopta ya Polisi ikiendelea na doria ya kuona kama kuna yeyote anaehitaji msaada kwa wakati huo.
Wengi walilazimika kutembea kwa miguu leo kwani hakuku na gari iliyokuwa ikiruhusiwa kupita katika eneo la Jangwani leo.
Wananchi wakisaidiana kushusha mtumbwi katika eneo la jangwani tayari kwa kazi ya kuokoa waliokwama kwenye mafuriko hayo.
Gari la wagonjwa likipita huku na kule kuona kama kuna yeyote anaehitaji msaada.
No comments:
Post a Comment