Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Eugen Mikongoti (katikati) akionyesha Tuzo ya Utoaji wa Huduma Bora za kijamii baada ya kuibuka na ushindi wa jumla katika mashindano ya Mashirika ya Hifadhi za Jamii kwa nchi za Ukanda wa Afrika,baada ya kukabidhiwa na Rais wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA) ,Bw. Errol Frank Stoove (kushoto) kwenye hafla fupi iliyofanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha usiku wa kuamkia leo.Kulia ni Muweka Hazina wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA),Philippe Conus.
Rais wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA) ,Bw. Errol Frank Stoove (kushoto) akikabidhi tuzo mbili za Utoaji wa Huduma Bora za Kijamii kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) William Erio (katikati) katika hafla fupi ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Mount Meru,jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi Serikali (GEPF), Daudi Msangi akipokea tuzo ya Utendaji Bora Afrika kutoka kwa Rais wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA) ,Bw. Errol Frank Stoove (kushoto) baada kushinda katika mashindano yaliyozishirikisha nchi 19 katika Ukanda wa Afrika. Kulia ni Mweka Hazina wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA),Philippe Conus.
Rais wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA) ,Bw. Errol Frank Stoove (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Eugen Mikongoti (pili kulia) ambaye Mfuko wake ndio Ulioshinda Tuzo ya jumla Utoaji wa Huduma Bora za Kijamii kwa Mashirika ya Hifadhi za Jamii kwa nchi za Ukanda wa Afrika,akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA),Bw. Hans-Horst Konkolewsky Pamoja na Mweka Hazina wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA),Philippe Conus.
Washindi wa Tuzo za Utoaji wa Huduma Bora za Kijamii wakiwa pamoja na Wadau waliowasindikiza kwenye hafla hiyo.
Furaha ya Ushindi ilitawala kwa Wakuu hawa.
Meza kuu.
Picha ya Pamoja wa Washindi woote wa Ukanda wa Afrika
No comments:
Post a Comment