Monday 9 January 2012

Dar Live Family Day ilivyobamba Mbagala


 Dogo Aslay wa TMK akiburudisha watoto wenzake.

ilikuwa ni soo wakati burudani ya kukata na mundu ilipoangushwa katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala - Zakhem jijini Dar es Salaam katika Siku ya Familia (Family Day).

Wasanii kibao walicharaza shoo ya ukweli juu ya jukwaa la kisasa la kupanda na kushuka na hivyo kukata kiu kwa mashabiki waliokuwa wakishangilia muda wote.
Wakali waliofanya kweli ni pamoja na Aslay Isihaka ‘Dogo Asley’ na Mwalami Hamis Kajonjo ‘Dogo Mu’ wa Familia ya Mkubwa na Wanaye, Bendi ya Extra Bongo, Crew ya JNY Unity, East African Melody Taarab na TMK Wanaume Family.

Ni shoo ya kijanja iliyowakutanisha wakazi kibao wa Jiji la Dar es Salaam ambapo watoto walijiachia kwa michezo mbalimbali huku wakipata misosi ya ukweli ilivyotayarishwa kitaalam.

Dogo Aslay anayekimbiza na ngoma yake ya Naenda Kusema aliwakonga vilivyo machalii wenzake ambapo kiduku kilichezwa si masihara.

Jioni ikawa ni zamu ya wakubwa ambapo Chege na Temba, Extra Bongo na wengine kibao waliangusha bonge la burudani na kuifanya Mbagala kuchizika ile mbaya.
Crew ya JNY Unity ilitia fora, ingawa ilikuwa ndiyo mara yao ya kwanza kupanda jukwaani kupiga shoo.

Mratibu wa Burudani wa Dar Live, Juma Mbizo alisema: “Huu ni mwanzo tu, tutaongeza burudani zaidi kila wiki, sasa shughuli imehamia Mbagala.”

 Ali Choki juu ya jukwaa.
 Extra Bongo wakifanya vitu vyao.
 Mwanahawa ally wa East Afican Melody akitumbuiza.
 Ali Choki stejini.
 Temba na Chege wa TMK.
 Mkubwa Fella wa TMK akiwa na Dj.
 Mnenguaji wa Extra Bongo jukwaani.
Mhe. Temba na mrembo wa mbagala.

No comments:

Post a Comment