Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gahrib Bilal akiongoza sala maalum ya kuombea marehemu mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Balozi Athumani Mhina, kabla ya mwili huo kusafirishwa leo kwenda Korogwe kwa mazishi. Shughuli hiyo ilifanyika nyumbani kwa marehemu, Wazo, jijini Dar es Salaam leo.
Vijana wa CCM wakibeba jeneza lenye mwili wa Balozi Mhina ulipowasili nyumbani kwa marehemu, Wazo ukitolewa hospitali ya Lugalo.
Masheikh na Wanazuoni wakisoma kisomo maalum cha kumuombea marehemu Balozi Athumani Mhina.
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Balozi Mhina, Wazo kabla ya kusafirisha mwili kwenda Korogwe, Tanga, leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Balozi Mhina, kabla ya mwili kusafirishwa kwenda Korogwe, leo.
Watibu wa Jumuia ya Wazazi Kinondoni, Stanley Mkandawile akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Tabora, Aden Rage, Mwenyekiti wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Azan Zungu na Waziri wa zamani, Iddi Simba, kwenye msiba huo.
Makamu wa Rais, Dk. Bilal akimpa pole Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi,Dogo Mabrouk.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa akitia saini kitabu cha maombolezo, nyumbani kwa marehemu Balozi Mhinam Wazo, Dar es Salaam, kabla ya shughuli ya kusafirisha mwili kwenda Korogwe Tanga.
Wanafamilia wakiwa katika majonzi wakati wa shughuli ya kusafirishwa mwili wa marehemu leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Wilson Msekwa, Katibu Mkuu wa CCM,Pius Mukama na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye wakizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omari Chambo wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Balozi Mhina, Wazo, Dar es Salaam, leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akimfariji, Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi (Zanzibar) Dogo Mabrouk wakati wa shughuli za kusafirisha mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuia hiyio Balozi Mhina, leo.
Waziri Nchimbi akifarijiana na Naibu waziri wa Nishati na Madini Adamu Malima (kulia) na Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa (katikati) kwenye msiba huo.
No comments:
Post a Comment