Monday 23 January 2012

Galileo Tanzania wazindua huduma mpya ya kuuza tiketi za ndege

Wafanyakazi wa Galileo Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya hafla ya uzinduzi wa huduma yao mpya ambayo inamuwezesha wakala wa kuuza tiketi za ndege kuuza tiketi kwa urahisi zaidi,uliofanyika kwenye ukumbi wa J.B Belmonte Selous ,Quality Centre jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Zamani wa Galileo Tanzania,Mwalim Ally akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kwa uzinduzi wa huduma mpya inayomuwezesha wakala wa kuuza tiketi za ndege kuuza tiketi kwa urahisi zaidi,uliofanyika kwenye ukumbi wa J.B Belmonte Selous ,Quality Centre jijini Dar es salaam.Wa Pili Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Sasa,Eliasaph Mathew.
Ofisa wa Mafunzo wa Galileo Tanzania,Gloria Urassa akitoa mafunzo ya namna huduma hiyo inavyotumika kwa Baadhi ya Mawakala wa Uuzaji wa tiketi za ndege nchini (Travel Agents) mara baada ya kuzinguliwa kwenye ukumbi wa J.B Belmonte Selous,Quality Centre jijini Dar es salaam hivi karibuni.
Ofisa wa Mafunzo wa Galileo Tanzania,Robert Maina akiwa katika muendelezo wa kutoa mafunzo ya namna huduma hiyo inavyotumika kwa Baadhi ya Mawakala wa Uuzaji wa tiketi za ndege nchini (Travel Agents) mara baada ya kuzinguliwa kwenye ukumbi wa Savannah Lounge,Quality Centre jijini Dar es salaam hivi karibuni.
Mwenyekiti wa TASOTA,Moustafa Khataw akizungumza machache mara baada ya uzinduzi huo.
Baadhi ya Maofisa wa Galileo Tanzania wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa TASOTA,Moustafa Khataw (hayupo pichani) wakati akizungumza na baadhi ya mawakala wa uuzaji wa tiketi za ndege hapa nchini wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya uuzaji wa tiketi.

No comments:

Post a Comment