Ludacriss akiwa na wasanii toka shoto: Mwasiti, Mwana FA, Ludacriss, Dogo Ditto, Joe Makini na Profesa J
Wiki hii wanafunzi kutoka shule mbalimbali hapa Dar es salaam walishuhudia muziki na kucheza muziki vyote vikifanya na vijana wenye vipaji wa THT ikiwa ni sehemu ya igizo la Hadi Lini lenye lengo la kuwaelimisha wanafunzi na jamii kwa ujumla umuhimu wa kujilinda dhidi ya Malaria, hii ni sehemu ya Kampaini ya Kitaifa ya Zinduka Malaria Haikubaliki!
Mwalimu Nkya kutoka Jangwani akizungumzia program hii alisema “njia hii ya kutumia sanaa inayofanywa kwa umahiri mkubwa na vijana wa THT inawezesha vijana na wanafunzi kujifunza kwa urahisi na kuhifadhi ujumbe wa mapambano dhidi ya malaria muda mrefu”
Leo tarehe 29 Julai, Wanafunzi kutoka Shule nne za Sekondari wanakutana na kushidana katika kuonesha michoro na picha, kuimba na mashairi yenye kuelimisha kuhusu Malaria. Mashindano haya ni sehemu ya kazi zinazofanywa na wanachama wa Zinduka Club, ambao ni wanafunzi waliopatiwa elimu thabiti juu ya malaria na ambao wako tayari kupeleka ujumbee huu kwa jamii. local communities. Majaji wamejionea vipaji mbalimbali vya wanafunzi na jinsi wanavyoweza kutumia mashairi, picha na nyimbo kuelezea namna ya kujikinga na kupambana na malaria.
Katika hatua ya fainali, wasanii wa Muziki wa Hip Hop na Mabalozi wa kujitolea wa Zinduka Prof Jay na Fid Q, walitumia wasaha huu kuzungumza na wanafunzi na kuwaelimisha umuhimu wa kujikinga na malaria kama njia ya kuhakikisha wanafikia ndoto zao na kutengeneza mustakabali mzuri wa maisha yao ya baadaye. Prof Jay na Fid Q wamekuwa watu muhimu katika kampaini hii ya Zinduka Malaria Haikubaliki, amabapo kwa pamoja walishirki katika uzinduzi wa kampaini hii Januari mwaka 2010, kampaini iliyozinduliwa narais wa Jakaya Kikwete .
Fid Q alikuwa na haya ya kusema ‘Nimejiunga katika kampaini nikiwa na matumaini kuwa kupitia muziki wangu naweza kusaidia mapambano dhidi ya Mlaraia nchina. Nianapotazama nia ya wanafunzi ya kujiunga katika mapambano ahaya na kutumia muziki kama jukwaa la kutolea ujumbe wa malaria kwa jamii, kwa kweli nafarijika na kujisikia fahari sana juu ya kazi tunayoifanya”
Wasanii hawa waliguswa na umati mkubwa wa wanafunzi, uliochangiwa na kuja kwa Ludacris ambaye atakuwepo kwenye Fiesta mwaka huu. Ludacris ambaye yupo nchini amehudhuria pia tamasha hili lililoandaliwa na wanfunzi, baada ya kusikia kazi kubwa inayofanywa na Zinduka nchini Tanzania.
Mwanafunzi Neema Frank kutoka Zanaki akielezea ujio wa wasanii alikuwa na haya ya kusema “Tumefarijika sana na ujio wa wasanii ambao mara nyingi tunasikia na kufuatilia kazi zao, leo wametufunza mengi na kutuhamasisha sana, tumetambua kuwa sisi ni sehemu muhimu ya mapambano dhidi ya malaria”
The Malaria Haikubaliki Campaign is led by the Tanzanian Government behind the leadership of President Jakaya Kikwete. It is supported by partners including Malaria No More, Tanzania House of Talent (THT), Johns Hopkins University, Population Services International and United Against Malaria. The goal of the program is to achieve universal bed net coverage and eliminate malaria deaths by urging all Tanzanians to Zinduka! (“Wake up!”) to the threat of malaria and protect themselves against the disease.
No comments:
Post a Comment