Tuesday 26 July 2011

SAFARI YA MWISHO YA DANNY MWAKITELEKO

Misa ya kumwombea Marehehemu Danny Mwakiteleko ilifanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Ndala. Na baade maziko kufanyika katika makaburi ya Masebe 1 kijijini Ndala, Kata ya Kandete, Tarafa ya Busokelo Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Danny alifariki Julai 23 kwa ajali ya gari na kuzikwa leo Julai 26, 2011.Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amen.
Aliyekuwa rafiki mpendwa wa Marehemu,Mpoki Bukuku akiweka shada la maua.





Muwakilishi wa Jeshi (JWTZ) kutoka Lugalo akiweka shada la maua.





Mhariri mtendaji wa Tanzania Daima na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ambaye pia alikuwa rafiki wa karibu wa marehemu Danny,Absalom Kibanda akiweka shada la maua.





 Mhariri Mtendaji wa New Habari, Deodatus Balile akiweka shada la maua.
Mwili wa marefemu ukifunikwa mara baada ya kuwekwa kaburini.
Mwili wa marehemu ukishushwa kaburini.
Familia ya Marehemu Danny ikitoa heshima zake za mwisho jioni ya leo kabla ya kufanyika mazishi.
Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka New habari wakitoa heshima zao mwisho mbele ya Mwili wa marehemu.
Mhariri mtendaji wa Tanzania Daima na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ambaye pia alikuwa rafiki wa karibu wa marehemu Danny,Absalom Kibanda akisoma risala fupi.
Mhariri Mtendaji wa New Habari, Deodatus Balile akizungumza maneno machache juu ya Marehemu Danny ndani ya umati mkubwa uliofika kanisani hapo jioni ya leo.
Meneja Mawasiliano ya ndani wa Serengeti Breweries (SBL) Iman Lwinga (kushoto) na Mkurugenzi wa Habari wa Bunge, Jose Mwakasukwa nao walishiriki.












































































































































No comments:

Post a Comment