Tuesday 19 July 2011

Mfuko wa michezo:Njohole legend foundation wazinduliwa jioni ya leo jijini dar.

Mgeni rasmi,Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Lut.Kanal Idd Kipingu pichani kati (shati la drafti) akiwa pamoja na familia ya Renatus Boniface Njohole,usiku wa leo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi ya michezo isiyo ya kiserikali alias Njohole Legend Foundation ndani ya hoteli ya Movenpick,jijini Dar.
 
 
Mgenirasmi,Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Lut.Kanal Idd Kipingu pichani kulia akimkabidhi cheti cha uthibitisho mchezaji wa mpira ambaye kwa sasa anachezea nje,Renatus Boniface Njohole,usiku wa leo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi ya michezo isiyo ya kiserikali alias Njohole Legend Foundation ndani ya hoteli ya Movenpick,jijini Dar.
Mgeni rasmi,Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Lut.Kanal Idd Kipingu akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa mfuko usio wa kiserikali wa Michezo,Njohole Legend Fouundation,Mfuko huo utalenga kuwasaidia wanamichezo mbalimbali wa hapa nchini kwa namna moja anyingine
 Pichani kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Wizara ya Habari,vijana utamaduni na michezo,Mh Juliana Matagu Gasoda akifafanua jambo kwa umakini jioni ya leo ndani ya hoteli ya Movenpick,wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfuko wa michezo usio wa kiserikali,Njohole Legend Foundation,na kushoto kwake ndiye mwanzilishi wa mfuko huo,Renatus Boniface Njohole.
Mwanzilishi wa mfuko huo usio wa Kiserikali,Renatus Boniface Njohole akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wanaadishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jioni ya leo,kwenye hafla fupi iliyopfanyika kwenye hoteli ya Movenpick,jijini Dar.
 Wageni waalikwa mbalimbali wakijadiliana jambo kabla ya uzinduzi rasmi kufanyika.
Pichani shoto ni Naibu Mkurugenzi wa Wizara ya Habari,vijana utamaduni na michezo,Mh Juliana Matagi Gasoda akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweries,Teddy Mapunda,jioni ya leo ndani ya hotel ya Movenpick.
Mtangazaji mahiri wa Clouds FM 88.4  Ephrahim Kibonde kupitia kipindi cha Jahazi,ambaye pia ndiye aliyekuwa akiongoza hafla ya uzinduzi wa mfuko wa michezo uitwao Njohole Legend Foundation.
 Nyota wa zamani wa soka waliokuwa ni baadhi ya wageni waalikwa wakijadiliana na kubadilishana mawazo. Toka shoto ni Kitwana Manara, Mdau. Mohamed Rishard Adolf, Mohamed Mkweche na Juma Pondamali



 Wageni waalikwa wakipata vinywaji laini laini kwanza kabla ya uzinduzi rasmi kufanyika.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya SBL.Teddy Mapunda,Naibu Mkurugenzi wa Wizara ya Habari,vijana utamaduni na michezo,Mh Juliana Matagi Gasoda,Meneja Mahusiano ya Jamii (SBL),Nandi Mwiyombela pamoja na Meneja Mahusiano ya ndani wa SBL,Iman Lwinga wakifuatilia hafla fupi ya uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment