Thursday 14 July 2011

uzinduzi wa tamasha la Utamaduni wa Oman hapo Bait -el ajaib mjini Zanzibar.

Makamo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Idd akitoa maelezo juu ya Uchoraji wa Hina kwa Balozi mdogo wa Oman Zanzibar, Sheikh Majid Abdallah huku Waziri wa Habari wa Zanzibar Jihad Hassan (mwenye kanzu) akisikiliza maelezo hayo katika Maonesho hayo Beit el Ajaib Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd akioneshwa dhahabu ya Oman kutoka kwa Afisa tamaduni wa Oman, Sheikh Ali Ahmed baada ya Balozi huyo kulifungua rasmi Tamasha hilo.
Wasanii wa kioman wakionesha umahiri wao wa kupiga ngoma za Utamaduni wa Oman kabla ya Ufunguzi wa Tamasha hilo Beit el Ajaib Mjini Zanzibar.
Kikundi cha ngoma kutoka Oman kikitumbuiza katika tamasha la Utamaduni wa Oman hapo Bait -el ajaib mjini Zanzibar.
Wasanii wa kioman wakicheza ngoma za Utamaduni wa Oman kabla ya Ufunguzi wa Tamasha hilo Beit el Ajaib Mjini Zanzibar.
PICHA NA HAMAD HIJJA-MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment