Monday 18 July 2011

Mashindano ya Airtel Rising Stars kuanza rasmi kesho jijini dar

 Kaimu Katibu Mkuu wa TFF,Sunday Kayuni akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa kufanya droo ya kupanga tariba ya mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 yafahamikayo kama AIRTEL RISING STARS ambayo yanataraji kuanza rasmi kesho katika viwanja mbali mbali vya jijini Dar es Salaam.Mashindano hayo yatashirikisha timu za kutoka mikoa ya kimichezo ya Kinondoni,Ilala na Temeke huku timu zingine zikitokea mikoa ya Morogoro,Mwanza na Iringa.Kushoto ni Kocha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars),Jan Poulsen.
 Meneja Mahusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania,Jackson Mmbando (katikati) akisisitiza jambo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) kabla ya kupangwa kwa droo ya mashindano ya AIRTEL RISING STARS yaliyozinduwa majuma kadhaa yaliyopita na mchezaji wa zamani wa timu ya Manchester United ya nchini Uingereza,Andy Cole alikuja hapa nchini.Kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Tanzania,Rahma Mwapachu na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa TFF,Sunday Kayuni.
 Meneja Mahusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando (kushoto) akikabidhi mpira kwa Mwalimu Zainabu Mbiro wa Shule ya Sekondari ya Twiga kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yanayotajaji kuanza kutimua vumbi hapo kesho katika viwanja mbalimbali.
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Airtel Tanzania,Rahma Mwapachu akikabidhi jezi kwa  Mwalimu Zainabu Mbiro wa Shule ya Sekondari ya Twiga.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Azania, Bernard Ngozya akikabidhiwa mpira na Meneja Mahusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando.
 Kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars),Jan Poulsen (kulia) akiteta jambo na Kocha wa Timu ya Taifa ya Vijana,Kim Pousen.
 Wakifatilia Droo ikichezeshwa.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakisoma majina ya timu zitakazoshiriki katika mashindano hayo.
Waandishi wa habari wakichukua vikaratasi ili kuchezesha droo ya timu na makundi yake.
Waandishi wa habari mkutanoni.

No comments:

Post a Comment