Kandanda
Wazazi wakionekana kufurahi na watoto wao katika mkusanyiko huo uliokutanisha Familia za Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kucheza pamoja, kula pamoja, kunywa pamoja na kushiriki michezo mbalimbali.
Familia zikiwa pamoja.
Mgeni rasmi Mkuu wa Itifaki Balozi A. Itatiro akizungumza machache wakati wa UN Family Day na kusema kwamba siku hiyo haikuwa ya kusoma risala bali ni siku ya kufurahi pamoja....Happy Birthday UN..!!!
JAMANI NYIE VIPI JIPANGENI BASI TUANZE JUA KALI: Ililfika zamu ya Wakubwa kupimana nguvu katika mchezo wa kuvuta kamba baina ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.
Timu ya Umoja wa Mataifa Vuta nikuvute....!!!
Ushindi ukaibukia kwa UN huku Wizara ya Mambo ya Nje ikala kwao.
Timu ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou akionekana kufurahishwa na ushindi wa Vijana wake.
MC akiongoza Wafanyakazi wenzake katika kucheza KWAITO.
Vikombe kwa ajili ya washindi wa mechi kati ya UN na Wizara ya Mambo ya Nje.
Pichani Juu Kapteni wa timu ya Mpira wa Miguu ya Umoja wa Mataifa akipokea kikombe cha ushindi wakati wa mchezo wa kuvuta kamba kwa niaba ya wafanyakazi wenzake kutoka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Itifika Balozi A. Itatiro. Chini UN Oyeee....
Kapteni wa timu ya Mpira wa Miguu ya Umoja wa Mataifa
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika picha ya pamoja na kikombe chao.
Menyu
Ongeza..Ongeza.....
Chilli sosi iko wapi jamani....
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Alberic Kacou (wa pili kulia) akiwa na Vijana wake wa kazi.
Kwaito...
Kwaito likiendelea
Hoyce Temu katika picha ya pamoja na binti ambaye angependa kuwa kama yeye hapo baadaye.
No comments:
Post a Comment