Thursday 3 November 2011

Kiota cha kisasa cha Msemo Hotels and Tours LTD mjini Mtwara

Mama balozi wa finland hapa nchini Tanzania Ms Sinikka Antila aliandaa chakula cha jioni katika hotel ya Msemo mjini Mtwara na kuhudhuliwa na watu wapatao 80 akiwemo Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Joseph Simbakalia na viongozi wengine waandamizi wa mkoa wa mtwara,waliohudhuria wengine ni maafisa waandamizi toka wizara ya mambo ya nje na ushurikiano wa kimataifa Tanzania pamoja viongozi wa finaland waliokua katika msafara.

Wageni walifurahi sana na hawakuamini kama wapo Mtwara kwa huduma bora ya kiwango cha hali ya juu na mandhari ya eneo husika. Msemo Hotels and Tours LTD ni hotel pekee ya kitalii ya kujivunia kwa mkoa wa Mtwara.

Chakula kilikua na mchanganyiko wa kiafrika na kimagharibi kwa kuzingatia afya ya mlaji. Fatilia picha utaona unadhifu wa fanyakazi na mazingira safi ya hoteli kwa mapumziko ya kifamilia au jumuiya.














No comments:

Post a Comment