Monday, 4 July 2011

kambi ya redd's miss ilala yaanza rasmi leo

 Mkurugenzi wa Dar Metropolitan Promotions ambao ni waandaaji Mashindano ya Redd's Miss Ilala,Jackson Kalikumtima (katikati) akionge na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo wakati wa kutangaza rasmi kambi ya Redd's Miss Ilala 2011 katika hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar es Salaam.Kulia ni Ofisa Udhamini wa Vodacom Tanzania,Ibrahim Kaude na kushoto ni Jesse Jackson wa Dar Metropolitan Promotions
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Buttallah (kushoto) akiongea na Warembo wanatakaoshiriki katika Mashindano ya Redd's Miss Ilala 2011 (hawapo pichani).
Miss Ilala 2010,Bahati Chande akiongea na Waandishi wa Habari.
Kikao cha Uongozi wa Redd's Miss Ilala 2011 na warembo washiriki kikiendelea katika hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Buttallah (pili kulia) akipena mkono na Warembo watakaoshiriki mashindano ya Redd's Miss Ilala 2011 na kuwatakia kila la kheri katika kambi yao inayoanza leo kwenye hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar.kulia ni Mrembo anaemaliza muda wake,Bahati Chande.
Mtaalam wa Mambo ya Habari wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu akipena mkono na Warembo watakaoshiriki mashindano ya Redd's Miss Ilala 2011.Kulia ni Msimamizi wa Warembo hao,Sylvia Shally.
Warembo wakiwa katika picha ya pamoja na Wasimamizi wao.
Baadhi ya Wanahabari wakiwajibika.
Warembo woote katika picha ya pamoja.

WAREMBO 21 wameanza kambi ya Reds Miss Ilala ilioanza jana katika hoteli ya Lamada, Dar es salaam.

Katika kambi hiyo warembo hao walianza kwa semina ya siku moja ambapo walielekezwa masuala mbalimbali muhimu ya kijamii.

Akizungumza katika semina hiyo mratibu wa Miss Ilala Jackson Kalikumtima aliwataka warembo hao kuwa makini na watu wanaoweza kuwaharibia sifa zao za kushiirki shindano hilo.

Alisema kuwa warembo wengine hushindwa kumaliza shindano hilo kutokana na kujikuta wakiwa katika kashfa na vitendo vuisivyokuwa na maadili.

Naye Meneja Masoko wa kampuni ya Bia Tanzania, Fimbo Butallah aliwataka warembo hao kujitambua na kuwa mstari wa mbele katika kuonesha maadili mema.

Alisema kuwa TBL kupitia kinywaji cha Reds imeamua kudhamini kanda tatu za Dar es salaam ambazo ni Ilala, Kinondoni na Temeke na kwa sasa mashindano hayo yatakuwa yakiitwa Reds Miss Ilala, Kinondoni au Temeke.

“ Ni kwamba kama ambavyo Reds ilivyo karibu na warembo au niseme akina dada kiujumla na ndivyo ambavyo naona kuwa hata ninyi mnatakiwa kuwa karibu na jamii na kuwa mfano katika jamii inayowazunguka” alisema Butallah.

Warembo hao ni Jenifer Kakolaki, Alexia William , Meryvine Kenzia, Patricia Kajubi, Salha Israel, Lilian Paul, Diana John’ Judith Mlingwa, Nasra Salim’ Cresencia Haule,Godliver Mwashamba, Williet Wilson,Faizal Ally, Priscilla Mchemwa, AugostinaMshanga, Ritha Cuthbert , Lilian Bryceson, Maria John, Lilian William, Edna Mnada,Mariam Manyanya.

Shindano hilo litafanyika Julai 29 (siku ya Vunja jungu) katika ukumbi ulioko katikati ya jiji la Dar es salam.
Wadhamini waliojitokeza kudhamini Shindano hilo ni Redds Original inayozalishwa na kiwanda cha Tanzania Breweries Limited ambao ndio wadhamini wakuu, wengine ni Vodacom Tanzania, Tanzania Standard Newspapers, Fabak Fashion, TV Sibuka, Maisha Club, na 88.4 Clouds FM na Paris Pub ya Tabata.

“ Watakapokuwa kambini warembo watajifunza mambo mbali mbali yanayohusu mashindano ya urembo, mambo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kibiashara. Pia watajifunza namna ya kujitunza kama wasichana na kufanya shughuli za kijamii.” Alisema Kalikumtima

No comments:

Post a Comment