Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust,Mama Salma Kikwete akizungumza kwa msisitizo wakati akitoa hotuba yake kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee,jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust ambaye pia ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani,Mh. Mwanaida Maajar akizungumza wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo ambayo inalengo la kusaidia swala la elimu nchini hasa kwa kuwakwezesha wanafunzi kusoama wakiwa wamekaa kwenye madawati mazuri.uzinduzi huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Karimjee,jijini Dar es Salaam.kushoto kwakwe ni mgeni rasmi Mama Salma Kikwete,akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo,Ndg. Shariff Maajar na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo,Bi. Zainab Sinare.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Trust,Balozi Mwanaid Maajar (kushoto) akipatia zawadi ya Maua Mgeni rasmi katika hafla hiyo,Mama Salma Kikwete.
Mwendeshaji wa Shughuli hiyo,MC Taji Liundi akionyesha picha maalum (logo) itakayokuwa ikitumiwa na Taasisi hiyo.
Mama Salma Kikwete akionyesha logo maalum ya Taasisi hiyo wakati akiizindua rasmi.
Mjumbe wa Bodi ya Taasisi hiyo,Dr. Maria Joseph Kamm akitoa shukrani zake kwa niaba ya Taasisi hiyo kwa Mgeni Rasmi pamoja na kwa wageni woote waliohudhulia hafla hiyo leo.
Wageni toka sehemu mbali mbali waliohudhulia hafla hiyo.
Kila mmoja alikuwa makini kusikiliza kilichokuwa kikizungumzwa katika hafla hiyo leo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar,Balozi Mwanaid Maajar akiongozana na Mgeni rasmi Mama Salma Kikwete kwenda kupiga picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi hiyo na watoto wa shule ya Msingi Amani ya Kinondoni ambayo ni moja ya shule zilizofanikiwa kusaidiwa na Taasisi hiyo.
Picha ya Pamoja na Viongozi.
Picha ya Pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Amani pamoja na walimu wao.
Ankal akiwa na Wadau.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete, leo Jumatatu amezindua taasisi isiyokua ya kiserikali ijulikanayo kama Hassan Maajar Trust (“HMT”), ikiwa na lengo la kusaidia sekta ya elimu nchini kwa kuanzisha kampeni yenye lengo la kukusanya shilingi bilioni 3 katika kipindi cha miaka 2 hadi 3 ijayo. Fedha zitakazochangwa zitatumika kwa ajili ya ununuzi wa madawati kwa shule za umma za msingi na sekondari ili kuboresha elimu nchini.
Kabla ya kuzindua nembo ya taasisi hiyo Mama Kikwete alisema kuwa taasisi hiyo imeanzishwa wakati muafaka kwa sababu “ni wajibu wa kizazi chetu kuhakiksha kwamba haitokei tena watoto wetu kukaa sakafuni wawapo madarasni mwao”
Akiongea wakati wa Uzinduzi wa taasisi ya HMT Balozi Mwanaidi Maajar, alisema, "Kampeni itaendeshwa kwa jina la Dawati kwa kila Mtoto au A Desk for every child kwa kiingereza, na kampeni hii itafanyika nchini Tanzania na Marekani. Uzinduzi rasmi wa kampeni hii utafanyika tutakapokaribia mwisho wa mwaka na tarehe ya siku ya uzinduzi huo itatangazwa mapema kabla ya siku ya tukio"
Mbali na kampeni hii ya "Dawati kwa kila mtoto",taasisi hii itajihusisha katika miradi mingine ya kusaidia vifaa vya shule ili kuboresha elimu na kuendeleza michezo.
Jina la HMT limekuja kwa heshima ya Hassan Shariff Maajar, aliyefariki mwaka 2006 kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea huko Mbabane, Swaziland.
HMT imeanzishwa na familia na marafiki wa Hassan, kama kumbukumbu yake na Hassan alikutwa na umauti akiwa na umri wa miaka 18 huko Mbabane, Swaziland alikokua akisoma katika chuo cha Waterford Kamhlaba United World College.
Hassan alikuwa kijana mmoja hodari, mahiri na mchapakazi ambaye alikuwa na shauku ya michezo na kutoa kwa ajili ya kusaidia jamii. Hassan alikua mchezaji wa mpira wa kikapu na alikua nahodha wa timu ya shuleni kwake hadi aliokutwa na umauti.
Hassan alipenda kusaidia jamii na muda mwingi alijitolea kufundisha michezo kwenye shule za watoto walemavu huko Mbabane, Swaziland.
Kwa kuutambua moyo huu, familia na marafiki zake tumehamasika kuunda taasisi hii kama kumbukumbu yake.
Takwimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinaonyesha kuwa shule za msingi na sekondari zina uhaba wa madawati na viti milioni 3.
Balozi Maajar alisema "HMT inaamini kuwa uhaba wa madawati mashuleni una athari kubwa kwa utoaji wa elimu nchini na tunatoa wito wa wadau wote tufanye juhudi zote ili kutatua tatizo hili”
Mwenyekiti alisema zaidi kuwa kuna uwekano mkubwa wa kumwezesha kila mtoto nchini kupata dawati na kiti katika kipindi cha miaka miwili hadi mitatu lakini suahal hili linahitaji mshikamano kwa kila mtu kutoka Nyanja tofauti na jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa kusaidia kufanikisha jambo hili.
"Tunatarajia kwamba watu kutoka nyanja zote za maisha watajitolea kupitia HMT kuchangia madawati," alisema Mwenyekiti wakati akiongea na vyombo vya habari.
Katika kampeni hii, HMT itatumia njia mbalimbali kukusanya michango, ikiwa ni pamoja na maombi ya moja kwa moja kutoka kwa wananchi na kwa kutumia vyombo vya habari ili kufikisha ujumbe kwenye jamii.
Tunahamasisha watu kuchangia chochote ikiwemo nguo, vyombo vya ndani, viatu, vitu ya watoto, vitabu, pia tunaomba makampuni kwa upande mwingine, kuchangia kutoa vitu wanavyotengeneza au huduma wanazotoa.
HMT imefungua duka la hisani pale jengo la Arcade, Mikocheni kwa ajili ya kuuza vitu mbalimbali vitakavyotolewa kama mchango ili kulipia gharama za uendeshaji kusudi fedha zote zitakazopatikana zitumike kwa ajili ya kununulia madawati.
Bodi ya HMT itaunda kamati ya kuchangisha fedha, ambayo itakuwa na jukumu la kutafuta fedha na kuhakikisha kwamba fedha zilizokusanywa zinahifadhiwa kwenye akaunti za benki za HMT na kutumika kwa kazi iliyokusudiwa. Kamati pia itakuwa na jukumu la kutoa taarifa kwa umma kila mwaka kuonyesha makusanyo na matumizi ikianisha idadi ya madawati yaliyopatikana.
No comments:
Post a Comment