Wachezaji wa timu ya Yanga,wakiongozwa na Nahodha wao Shadrack Nsajigwa wakishangilia ubingwa wao walioupata jioni hii kwa kuwachabanga bao 1-0 watani wao wa jadi Simba Sc katika mashindano ya Kagame-Castle Cup 201.
Waziri wa Habari,Vijana,Michezo na Utamaduni,Mh. Emmanuel Nchimbi akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Yanga,Shadrack Nsajigwa kitita cha dola za Kimarekani elfu 30 ikiwa ni zawadi ya ushindi walioupata leo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,David Minja (kushoto) akimvisha medani mmoja wa wachezaji wa timu ya Al Mereikh ambao ndio walioshika nafasi ya tatu ya mashindano hayo.
Wachezaji wa Simba wakipita kuchukua medali pamoja na zawadi ya ushindi wa pili.
Kipa wa timu ya Simba,Juma Kaseja akiwa karuka juu kudaka mpira uliokuwa ukielekezwa langoni kwake.
Mchezaji wa timu ya Simba,Kelvin Yondani (shoto) akikabana na mchezaji wa timu ya Yanga,Davies Mwape katika mchezo wa fainali za Mashindano ya Kagame-Castle cup uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mshambuliaji wa pembeni wa timu ya Yanga,Rashid Gumbo akichanja mbuga katika lango la timu ya Simba.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa na mpaka kupelekea ubingwa wa mashindano haya kuelekea mtaa wa Jangawani na Twiga leo.
Mashabiki wa Yanga leo kwao ni sikukuu kubwa sana maana ni furaha mwanzo mwizo.
Mashabiki wa Simba hali ilikuwa hivi.
Kocha msaidizi wa Yanga,Fred Felix Minziro akimlalamikia muamuzi kuwa anaongeza muda mwingi sana katika dakika 30 za ziada.
Mpiga picha wa Magazeti ya Tanzania Daima,Joseph Senga akilazimishwa kuondoka upande wa mashabiki wa timu ya Simba kwa madai kwamba amevalia nguo yenye rangi ya njano.jamani hivi hii kweli ni halali??
Upande wa Yanga nako walianza kuwatupia makopo watu wa huduma ya kwanza wakidaiwa kuwa wamevalia nguo zenye rangi ya timu ya Simba.
Hivyo nao walilazimika kuondoka uwanjani hapo kama wanavyoonekana hapa.
Baadae waliombwa kurudi na ikabidi woote wakae sehemu moja ambayo ni ya upande wa Mashabiki wa Simba.
No comments:
Post a Comment