Monday 11 April 2011

yanga yawasili jijini dar mchana huu na mwali wao mkononi

Kombe la Ubingwa wa ligi kuu lililonyakuliwa na Yanga mara baada ya kuitumgua timu ya Toto Afrika ya jijini Mwanza jana.
Nahodha wa Timu ya Yanga akiwa na mwali wao mara baada ya kuwasili jijini Dar mchana huu.
Msafara wa Kutoka uwanja wa Ndege wa J.K Nyerere kuelekea klabuni kwao ukianza.
Kocha mkuu wa Timu ya Yanga,Sam Timbe akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa J.K Nyerere kutokea jijini Mwanza walikokuwa wameenda kucheza mchezo wao wa kumalizia ligi kuu na kuunyakua ubingwa wa ligi hiyo kwa mwaka 2010/11.
Nahodha wa timu ya Yanga,Shadrack Nsajigwa (FUSSO) akiongea na vyombo vya habari juu ya ubingwa walioupata huko jijini Mwanza jana,katika uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere mchana huu.
Baadhi ya wachezaji na viongozi wa Yanga wakitoka uwanjani hapo kuelekea kwenye magari yaliyoandaliwa kwa ajili ya safari ya kwenda klabuni.
Mdau Ellihuruma Ngowi wa Vodacom akiwa na mwali huyo mchana huu.
Nahodha Nsajigwa akilibusu Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu.
Mashabiki wakilazimisha kumsaidia kombe nahodha wao,Shadrack Nsajigwa katika uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere mchana huu.
Mwali ameshawasili......
Mwenyekiti wa Yanga,Lloyd Nchunga akipiga stori na mmoja wa mashabiki wa timu hiyo.
Shabiki wa Yanga akiongea kwa mifano kwamba wamewachinja wapinzani hao kwa kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu.
Hapa ni Yanga Damu........
yaani ni furaha mtindo mmoja kwa mashabiki wa timu ya Yanga.
Msafara.
Poo Poo poooooo...........
Msafara.
Tarumbeta hapa ndio mahapa pake,yaani nyimbo zoote waliziimba.
Bi mkubwa mshabiki wa Yanga na wajukuu zake.
Mapokezi yakiwa yamepamba moto.
Mdau Zahor akitatua vurugu za ugawaji wa T-Shirt za ubingwa zilizokuwa zikigawiwa uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment